Kaka wa Nick Minaj akutwa na hatia ya ubakaji - teknomovies
Kaka wa Nick Minaj akutwa na hatia ya ubakaji

Kaka wa Nick Minaj akutwa na hatia ya ubakaji

Share This
Takriban wiki tatu zilizopita tuhuma za ubakaji zilimuandama kaka wa Nick Minaj Jelani Maraj. Upelelezi uliofanywa umemtia hatiani kuwa ana kesi ya kujibu juu tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ni kwamba uamuzi huo umetolewa siku ya jumanne Long Island. Jelani amekutwa na hatia ya kulazimisha penzi kwa mtoto na kuhatarisha ustawi wake.

Kutokana na tuhuma hizo Jelani anaweza kukumbana na adhabu hadi ya miaka 25 gerezani na hukumu yake itasikilizwa Dec 24.

ANGALIA : PICHA : MEEK MILL AKIWA KWENYE VAZI LAMFUNGWA

Nick Minaj amesema hajawahi kumuona kaka yake akifanya vitendo kama hivyo ingawa jambo hilo linawezekana. lakini kwa kumtetea kaka yake amesema shemeji wake wa zamani anatumia mbinu hiyo ili atajirike na fidia ya mamilioni.

Wiki kadhaa zilizopita mtoto wa kambo wa Jelani alitoa ushuhuda wa namna ambavyo baba yake huyo alivyotaka kum'baka tangu akiwa na miaka 11.
Kwa sasa ana miaka 13 na amezungumza yote aliyokuwa anafanyiwa na Baba yake huyo ambapo amesema kuwa alimtisha endapo atamwambia mama yake. Lakini pia alimwambia afanye nae mapenzi kinyume na maumbile (anal sex).

Sasa unaweza kudownload Teknomovies App kwenye google playstore ili uwe wa kwanza kupata story kali.


No comments:

Post a Comment

Pages