Uchambuzi : Ni kweli Despacito Haikustahili kupewa tuzo ya wimbo bora? - teknomovies
Uchambuzi : Ni kweli Despacito Haikustahili kupewa tuzo ya wimbo bora?

Uchambuzi : Ni kweli Despacito Haikustahili kupewa tuzo ya wimbo bora?

Share This
Kuna nyakati unashindwa kuwaelewa kabisa mashabiki wanataka nini. Wanaweza kukushangilia lakini muda huo huo wakakupiga mawe. Ndicho walichofanyiwa Luis Fonsi na Daddy Yankee kupitia wimbo wao wa Despacito kwenye tuzo za Grammy ambazo zimefanyika mwishoni mwa wiki.
Wimbo wa Despacito uliteka hisia za watu duniani kote, sio Marekani, Uingereza au Latin Amerika bali ni duniani kote. Binafsi nilipoona kipengele cha wimbo bora wa mwaka nilidhani Despacito itaibuka na ushindi huo. Sababu kubwa iliyonifanya niamini kuwa Despacito itaibuka na ushindi ni kutokana na wimbo huu ulivyosumbua kwenye soko la burudani kwa muda wa mwaka mzima tena wimbo ambao umeimbwa kwa lugha ya Kihispania ni aghalabu kupendwa kiasi hiki.

Akili yangu iliwaza ni wimbo gani mwengine katika kipengele hiki ambao umefikisha idadi ya watazamaji Billioni 4 mtandaoni? ni wimbo gani umeweza kuwaunganisha watu wote wauelewe wimbo wenyewe bila kujali lugha zaidi ya Despacito? Hakika nilijiwekea aslimia 100 kuwa Luis Fonsi atabeba tuzo lakini haikuwa hivyo badala yake tuzo ikaenda kwa Bruno Mars na wimbo wake wa "That's What I Like".

Achana na kipengele hicho tazama kipengele cha Record of the year ambacho Despacito pia ilikuwa ikigombea nilikuwa na uhakika wanachukua na sababu zangu ni kwamba Despacito imeweza kuwa downloaded duniani kote, imeweza kusambaa sehemu kubwa na pia watu walifurahia mashairi yake na kudiriki kuyaimba mara nyingi hii ilionyesha ni jinsi gani wimbo ulipata umaarufu .

Pamoja ya kuwa Justine Bieber alitoa support kwenye remix lakini ukweli ni kwamba hata asingekuwepo bado wimbo ungesimama kama ulivyo kwani Despacito haukuwa wimbo wa Kingereza wa Kihispania au wa Kilatini bali ulikuwa wimbo uliokusanya lugha zote duniani kwenye dakika 4 tu za mashairi. Lakini kwa mara nyingine tuzo ikaenda kwa Bruno Mars na rpund hii ilikuwa ni "24k Magic".

Kwa upande mwengine unaweza kudhani kuna figisu zinafanyika kwenye tuzo hizi kwani historia inaonyesha ni mara moja tu kwa wimbo ulioimbwa kwa lugha ambayo si Kingereza kushinda tuzo ya wimbo bora wa mwaka ambapo ilikuwa mwaka 1959 msanii Domenico Modugno's alishinda kupitia wimbo wake wa "Nel Blu Dipinto Dli Blu".

Kwa uelekeo huu inawezekana wimbo wa Despacito uliwekwa kwenye kinyang'anyiro sababu hakukuwa na namna kwani wasingeuweka wangekuwa hawajautendea haki lakini pia Despactico ilistahili kushinda tuzo kwani ni wimbo ambao una sifa zote za kushinda tuzo.

Kuna kitu kikubwa tumejifunza kupitia tuzo hizi, wazungu wanajijali wao wenyewe hawawthamini kabisa watu wengine. Ni mtu asiyejua muziki pekee ambae atapinga Despacito isipate tuzo.




No comments:

Post a Comment

Pages