CAMILA CABELLO NYOTA MPYA AMBAYO WENGI BADO HAWAJAIGUNDUA - teknomovies
CAMILA CABELLO NYOTA MPYA AMBAYO WENGI BADO HAWAJAIGUNDUA

CAMILA CABELLO NYOTA MPYA AMBAYO WENGI BADO HAWAJAIGUNDUA

Share This
Leo  nilikuwa napita pita kutazama baadhi ya Nyimbo mpya na baadhi ya wasanii wapya kupitia mtandao wa Youtube. Katika Kupita pita nilitua kwa huyu mrembo anaefahamika kwa jina la Camilla Cabello na kolabo yake pamoja na mtu mzima Young Thug inaitwa Havanna.
Niliposikiliza na kutazama kideo, Ambacho hakika ni Bonge moja la Kideo nimependa haswa namna Script ilivyochorwa yani ni kama unatazama Filamu fulani nzuri sana.

SOMA PIA>>FBI KUMCHUNGUZA JAJI ALIYETOA HUKUMU YA MEEK MILL

Sikua nikimjua Vizuri lakini nilipotafuta zaidi nyimbo zake nikagundua kuwa Nyimbo zake Nimewahi kuzisikiliza lakini sikuwa nikimjua kama ndio yeye aliyeimba.

Stori Yake Kwa Ufupi.

Kazaliwa Mwezi machi, Tarehe 03 mwaka 1997.Ana Uraia wa Cuba na pia Marekani ambapo Kiasili alizaliwa Cuba,Mashariki mwa Jiji la Havana katika mji unaofahamika kwa jina la Cojimar.

SOMA PIA>>ED SHEERAN BEYONCE ANABADILI BARUA PEPE KILA WIKI

Kwa sasa anaishi Miami pamoja na Wazazi wake ambako walihamia tangu akiwa na Miaka mitano. Alianza kufahamika haswa baada ya Kushiriki katika Shindano la X-Factor mwaka 2012 ambapo Yeye pamoja na wenzake watatu waliunganishwa kwa pamoja na Kuunda kundi lililofahamika kwa jina La The Fifth Harmony.
Fifthy  Harmony
Ukitafuta katika Mtandao wa Youtube au Google, Fifth Harmony basi utapata Nyimbo zao kali Japo mimi naipenda Cover Moja walifanya wakiwa pamoja na Boyce Avenue..Wimbo wa Justin Timberlake Mirrors..Bonge moja la Cover.

SOMA PIA>>WAHINDI KUJA NA FILAMU YA RAMBO KIVYAO

Turudi kwa Camila, Ambae huyu Mwezi Desemba mwaka 2016 aliamua kujitoa na kuanza harakati kama Solo.

Ana Nyimbo baadhi Kali..Bonyeza Hapo Chini Kuzipakua Baadhi nimekuwekea..

I Know I DiD Last Summer And Shawn Mendes

Havana Ft Young Thug

Real Friends

I Have A Questions.

Lakini ngoma ambayo Inakimbiza kwa sasa ni Havana ambayo imeachiwa August 03, na mpaka sasa imetazamwa na watu Milioni 300, Mwaka 2018 kashatangaza Ujio wa Albamu yake ambayo kaipa Jina la Camila

Tazama Hapa Chini Video Hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages