Tangazo Kwa Wapenzi wa THE ORIGINALS - teknomovies
Tangazo Kwa Wapenzi wa THE ORIGINALS

Tangazo Kwa Wapenzi wa THE ORIGINALS

Share This
The OriginalsSeries kali toka chaneli ya The cw "The Originals" imetangazwa kua season ya 5 ndiyo itakua ya mwisho kuachiwa.

Tangazo hilo lilitolewa na Muandaaji mkuu wa Series hiyo Julie Plec katika mtandao wake wa Twitter alhamisi hii.

Anasema ilitakiwa Watangaze kutoka mwaka mmoja nyuma hata kabla ya Tangazo la mwisho kwa Vampire Diaries.

Series ya The Originals, ni series iliyojizolea umaarufu mkubwa sana, iliyotokana na The Vampire Diaries mwaka 2013 na mpaka sasa zipo Seasons 4 huku kukiwa na Episodes 79 tu.

The originals kwa mwaka 2017-2018 toka pande Za The cw ilikua moja ya Series nayo iliyopata bahati ya kurudi hewani, ikiungana na The Flash, Supernatural, Arrow, Izombie, Dc Legends of Tomorrow na Jane the virgin.

Pages