Liam Neeson Kastaafu Filamu Za Ngumi,Anamaliza na Hii. - teknomovies
Liam Neeson Kastaafu Filamu Za Ngumi,Anamaliza na Hii.

Liam Neeson Kastaafu Filamu Za Ngumi,Anamaliza na Hii.

Share This
Mkali wa Taken, Liam Neeson ndo kaachia ngazi hivyo kwa kile anachodai Umri umekwenda hivyo Kwa upande wa filamu za mapigano anausahau kabisa.

Alisema hayo katika usiku wa Toronto Festival, kuwa umefika mwisho kwa upande wa filamu hizo ambazo ndizo zinazimwingizia mpunga mrefu na hivyo kuangalia upande mwingine zaidi.

"Wanazidi kunipa hela tu, mimi nawaambia sahizi nina miaka sitini na upuuzi mtanifukuzia mashabiki, " aliongeza.
Taarifa hii ya kuachia ngazi katika filamu za mapigano inaweza kuwa mshtuko kwa wengine, lakini kuanzia mwaka 2015 Liam alisema juu ya mipango yake ya kutundika daruga.
"Nafikiria miaka miwili mbele,Kama Mungu atanipa uhai zaidi naweza nikaacha filamu za namna hii nafikiri, " aliyasema hayo wakati akihojiwa na mwandishi wa The Gurdian.

SOMA PIA:WEMA NAUCHUKIA UMAARUFU

Mchongo wake mpya unaokuja ni "Hard powder" ambao unatarajiwa kuachiwa mwaka 2018.

Umepokeaje taarifa hii?Usisahau kutuachia maoni yako hapo pia kutufuata katika mitandao ya kijamii Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Habari mbalimbali.

Tazama Hapo chini Moja Ya Kipande Ambacho Kinapendwa Sana na Wengi Kutoka Kwake Kupitia Filamu Ya Taken

   

Pages