Fahamu Jinsi Ya Kudownload Status Ya Mtu WhatsApp Bila Yeye Kujua#Maujanja - teknomovies
Fahamu Jinsi Ya Kudownload Status Ya Mtu WhatsApp Bila Yeye Kujua#Maujanja

Fahamu Jinsi Ya Kudownload Status Ya Mtu WhatsApp Bila Yeye Kujua#Maujanja

Share This
Baada ya kuongeza kipengele kipya cha WhatsApp Status ambapo humuwezesha mtu kuweza kuweka picha na pia video fupi ambazo hupotea baada ya masaa 24,kuna Muda unaweza kupenda kitu cha rafiki yako ambacho kaweka katika Status yake na ukatamani ukimiliki lakini shida huja,Ni lazima umuombe yeye sababu hakuna Option ya kukuruhusu kuchukua.

Lakini kwa sasa tambua Unaweza kuchukua Status ya mtu bila hata kumwambia akutumie kwa kutumia njia mbalimbali na ukapata katika ubora mkali tu na ukaepusha usumbufu wa kuhitaji kutumiwa.

Ili kuweza kuchukua Status ya mtu fuata njia zifuatazo,Ambapo utaweza kushusha Picha,Video pamoja na Gifs.

1.Fungua WhatsApp yako alafu nenda sehemu ya kuangalia Status  mbalimbali.
2.Tafuta Status ya mtu unayohitaji kuichukua Kisha bonyeza kama unataka kuitazama.


3.Baada ya kufanya hivyo funga WhatsApp yako na kisha nenda katika File Manager yako,Kwa lugha nyingine nenda katika Memory Card yako.

4.Baada ya kuingia katika File Manager yako au Memory Card yako sasa fanya kutafuta Folda la Whatsapp.
5.Baada ya kufungua Whatsapp Folda lako nenda katika sehemu ya Media kama unavyoona katika Picha.
6.Baada ya kubonyeza hapo,Kitachofuata ni kutafuta Folda la "Statuses" ambalo huwa linakuwa linafichwa hivyo kuliona,Utabonyeza alama ya Option kisha Utaenda katika sehemu ya Hidden Files ili kulipata Folda 
hilo.
7.Sasa utaweza kuona Folda la Statuses Na ukibofya utaweza kuona Status mbalimbali ulizoweza kutazama,ambazo huwa zinakaa hapo

 8.Kitachofuata Sasa ni Kutafuta picha ambayo unaitaka,Na itabidi kuichukua picha na kuihamisha eneo lingine ambapo itabidi Uishikilie picha hiyo kisha Option kadhaa zitatokea,Wewe utachagua kui Copy ili tuweze kuihamisha.


9.Baada ya Ku copy hiyo picha rudi tena nyuma katika File Manager yako,Tafuta Folda la DCIM ambalo ni maalumu kwaajili ya picha lakini sio lazima hilo sehemu yoyote au unaweza kutengeneza Folda lingine kisha ukiingia hapo katika Folda fanya Kuipaste eneo hilo.
10.Baada ya kupaste hapo,Nenda Sasa katika Gallery yako alafu peruzi,Utaweza kuiona picha yako.

Sasa unaweza Kuiona picha yako,na unaweza Kushare na Washakaji Pia Hiyo picha kulingana na mahitaji yako ambayo ulikuwa unahitaji.

Note:Katika File Manager kuna Kutofautiana muonekano na pia Option,kama Hiyo ambayo nimetumia ni File Manager ya Simu yenyewe au Memory Card ya Simu yenyewe na sio Memory Card ya nje ambayo inaweza kuwa na Option tofauti lakini njia inabaki Kuwa Ile Ile.

Hapa Chini pia Unaweza kutazama Video kama Maelezo Hayajakuingia Fresh.

          

                      

Pages