Beka Flavour:Aslay Hata Kidogo Hanitishi#Mahojiano - teknomovies
Beka Flavour:Aslay Hata Kidogo Hanitishi#Mahojiano

Beka Flavour:Aslay Hata Kidogo Hanitishi#Mahojiano

Share This
Baada ya kundi lao, Ya Moto Bendi kuvurugika mpaka sasa Aslay na Beka Fleva  ndio majina pekee ambayo yameendelea kusikika masikioni mwa watu wengi kutokana na ngoma kadhaa ambazo kila mmoja ameziachia.
Ukiachana na hilo,mara kadhaa wamekuwa wakipambanishwa na mashabiki mbalimbali ambapo mpaka timu Aslay na timu Beka zimeanza kujitokeza.

Teknomovies ilifanya mahojiano na Beka Fleva ambapo alianza kwa kuzungumzia ushindani wake na Aslay ambao unafanywa na mashabiki wa Muziki ambapo anasema kuwa mashabiki wengi wanakosea sana kufanya hivyo.

“Huwezi kumpangia shabiki kufanya jambo fulani,lakini sio vizuri kunipambanisha mimi na Aslay kwanza sisi ni kama ndugu nab ado tuna wasiliana na tunaongea mambo mengi sana,” alisema

Ilikuaje dili mpaka Ya Moto

Beka anafunguka kuwa kwa mara ya kwanza alikutana na Mkubwa Fella,Morogoro ambapo alimuoneshea kipaji chake cha kuimba na Fella alipenda ambapo alimpatia namba ya simu kwa sababu kwa kipindi hicho bado alikuwa anasoma.

“Nilikuwa nawasiliana nae,mpaka nilipomaliza shule nilikuja Dar,nikaanza mazoezi Temeke ambako ndipo kuna kituo cha Mkubwa na Wanawe,baada ya hapo nikachukuliwa nikaanza kukaa hapo hapo,”
“Mwaka 2013 ndipo kundi liliundwa nakumbuka na hapo ndipo tulianza kuonekana na kufahamika na wengi baada ya kutoa kazi yetu ya kwanza ambayo iliitwa Ya Moto,na huo wimbo ndio ukawa chanzo mpaka la jina hilo la bendi,”

Changamoto

Beka anafunguka kwa sasa changamoto kubwa kwake ni anatakiwa kuimba sana na kuhakikisha anaachia ngoma kali zaidi.

“Wakati tukiwa Ya Moto tulikuwa na nyimbo nyingi lakini kwa sasa nipo peke yangu hivyo inanibidi nifanye kazi kwa bidii ili mashabiki zangu wafurahi,”

“Pia kingine changamoto kubwa kwa sasa inabidi pengine niachie ngoma nyingi,kwa sababu nikienda kwenye shoo kuna changamoto kubwa ya kupafomu nyimbo zangu ni chache sana,”anaongeza

Kama sio Muziki angekuwa anafanya nini kingine.

“Mimi kama sio muziki basi kwa sasa nafikiri ningekuwa nalima Mpunga nyumbani maana elimu nilizingua kwahiyo nafikiri ndio biashara pekee ambayo ningekuwa nafanya,”

Mahusiano kwake vipi?

Beka anafunguka kuwa mpaka sasa ana mpenzi ambae bado hajaamua kumuweka wazi na hata yeye mwenyewe bado ajataka kutambuliwa rasmi.

“Yeah yupo mtoto bhana,Nampenda sana lakini nafikiri bado muda wa kumuweka wazi nafikiri sio muda sana anaweza kuwekwa wazi,”

Matarajio yake.

Beka anazidi kufunguka kuwa anatamani kuja kufikia levo za kuitangaza Bongo kimataifa zaidi kwani anaamini uwezo huo anao wa kufanya hivyo.

“Na pia nina mpango wa kuja kusaidia wasanii wengine pia,natamani sana kumiliki wasanii na mimi naimani nitatimiza ndoto hiyo,”aliongeza

Yupo tayari kurudi Ya Moto?

“Mimi binafsi sipo tayari kurudi tena,sababu kwanza kwa sasa nina uongozi mpya unaonisimamia pamoja hata na akina Aslay na wengine pia wana uongozi wao sifikiri hilo linaweza kutokea,”

“Mimi kwa sasa ninasimamiwa na Siraji Issa ambae ndiye meneja wangu na John Sambila huyu ananisaidia sana katika masuala ya kifedha,” aliongeza

Shoo ambayo hawezi kusahau

“Kuna shoo siwezi kusahau ilikuwa Tanga kipindi hicho ndio tunawasha moto kweli kweli,nakumbuka ilikuwa Mwaka 2015,”

“Sasa kwenye huo ukumbi watu walijaa sana alafu AC(Viyoyozi) zilikata aisee tupo tunapafomu pumzi ikawa inakata kabisa,alafu watu shangwe la kutosha,”

“Ilitubidi tuombe kusimama kidogo ili tutoke nje kwenda kupata hewa ila nilikuwa najihisi kama nakufa alafu watu huku ndio hawana habari kabisa,”

Pesa yake ya kwanza alifanyia nini?

Beka anaendelea kufunguka kuwa pesa yake ya kwanza kabisa kuipata alituma nyumbani kwaajili ya kukarabati nyumba yao.

“Nakumbuka ilikuwa Milioni mbili na laki sita ambapo nilipoipata tu,nilituma nyumbani ili warekebishe nyumba na mambo mengine,”

Kitu anachojutia sana.

Beka anafunguka zaidi kuwa katika kitu anachojutia sana,ni kuwahi kuyajua Mapenzi jambo ambalo lilifanya kuharibu baadhi ya ndoto zake.

“Nakumbuka nikiwa nasoma kipindi hicho kuna msichana nilimpenda sana,lakini yeye alikuwa ananizingua nakumbuka alikuwa anaitwa Patricia,”

“Yani Yule msichana alinipeleka sana,nakumbuka kuna muda nilikuwa najifelisha makusudi kabisa ili anione kwa jinsi ninavyomfikiria alafu nilikuwa najiona kabisa niko poa lakini kwa sasa nagundua nilikuwa nafanya ujinga mkubwa sana,”

Kuhusu Nyimbo zake.

Wasanii wengi kwa sasa huwa wanatunga nyimbo zao na wengine kutungiwa ambapo kwa upande wake Beka anasema yeye hajawahi kutungiwa wimbo mpaka sasa anatunga mwenyewe.
“Nina nyimbo zaidi ya kumi na tisa mpaka sasa,zote nimetunga mwenyewe hakuna ambayo kuna mtu kanisaidia kuandika,”

Pia aliongeza zaidi kuhusu video zake ambapo anasema video ya Nibebe alifanyia Dar na Sikinai alifanyia mkoani Arusha.

Bifu na Aslay?

“Sina bifu na Aslay sisi bado ni ndugu na pia watu wanaongea sana kwamba Aslay anavyofanya nyimbo nyingi,eti ananitisha mimi,Kiufupi hanitishi sababu ndio utaratibu wake na mimi pia nina utaratibu wangu nafikiri watu wanaona kwa jinsi hali inavyokwenda,”

Anachokikumbuka Ya Moto

“Nimekumbuka sana,kwa jinsi tulivyokuwa tunaishi yani muda mwingi ilikuwa ni furaha sana hasa kipindi tukiwa tunaenda kwenye shoo,lakini kwa sasa naenda kwenye shoo najikuta nipo peke yangu,nakumbuka sana,”

Wasanii anaowakubali.

Anawataja wasanii Christian Bella pamoja na Vanessa Mdee ambao anasema wanamkosha sana na yupo mbioni kufanya nao kazi na anaamini zitafanya vizuri sana.
Mchango wa Diamond.

Ukiachana na Mkubwa Fella,Beka pia anamtaja Diamond Platnumz kuwa anamchango mkubwa sana kwao.

“Jamaa alikuwa mara nyingi anasisitiza tufanane na nyimbo zetu yani tujitengenezee namna ya kuonekana wa thamani,”

“Maana kwa jinsi tulivyokuwa tulikuwa hatufanani kabisa na nyimbo zetu,kila mara alikuwa anasisitiza hilo na pia alituunganisha kwenda kushuti nje kwa GodFather kilikuwa kitu poa sana.

Mahojiano haya yalifanyika kati ya Beka Fleva na mwandishi pia mhariri mkuu wa Teknomovies,Frank Daxx




Pages