Young Dee: Kiutani Utani Kama Lissu - teknomovies
Young Dee: Kiutani Utani Kama Lissu

Young Dee: Kiutani Utani Kama Lissu

Share This
NGOMA ya moto kwa sasa mtaani huwezi kuacha kutaja wimbo wa Young Dee unaokwenda kwa jina la Kiutani Utani ambao ameachia wiki hii kwa pamoja audio na video.

Katika mahojiano na Teknomovies Blogu juu ya wimbo huo Young Dee anasema wazo la wimbo huo lilikuja kutokana na ishu inayoendelea kwa sasa nchi ambayo huanza kiutani na baadae kuja kuwa jambo kubwa sana.

“Angalia ishu kama ya Diamond na Ommy Dimpoz ilianza kiutani utani tu afu baadae ikaja kuwa kitu kikubwa mpaka mambo ya ndani yakaanza kuongelewa pia angalia ishu ya Tundu Lissu nayo hivyo hivyo ila baadae ndio kama hivi inavyoonekana,” alisema.

Aidha Young Dee kaongeza pia watu wategemee midondoko mingine mingi zaidi sababu mwaka huu kabla haujaisha anataka kufanya mambo makubwa zaidi.

“Kwanza nawaomba radhi watanzania kwa kilichotokea hivyo ombi la msamaha wangu litaonekana zaidi kwa kazi nzuri,” alimaliza


Video ya ngoma hiyo katika mtandao wa Youtube mpaka sasa imeweza kutazamwa na watu zaidi ya laki moja na inatazamiwa kuzidi zaidi ya hapo sababu ndio kwanza ina siku nne tangu iwekwe Youtube.

No comments:

Post a Comment

Pages