Meek Mill kahamishwa gereza na sasa yupo kwenye gereza la wafungwa mchanganyiko - teknomovies
Meek Mill kahamishwa gereza na sasa yupo kwenye gereza la wafungwa mchanganyiko

Meek Mill kahamishwa gereza na sasa yupo kwenye gereza la wafungwa mchanganyiko

Share This
Kufuatia maombi ya kuhamishwa Gereza, kutoka kwenye gereza la faragha na kwenda kwenye gereza la wafungwa mchanganyiko sasa imefahamika kuwa maombi hayo yamesikilizwa na sasa Meek Mill yupo kwenye gereza ambalo linajumuisha wafungwa wa makosa tofauti.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ kwa sasa Meek Mill amehamishwa kwenye gereza la Camp Hill huko Chester ambapo anajichanganya na wafungwa wengine.

Awali Meek Mill alifungwa kwenye gereza la faragha kutokana na usalama wake kwani maafisa usalama walihisi huenda angechanganywa na wafungwa wengine angedhurika lakini mwanasheria wa Meek Mill aliandika barua kuomba Meek Mill achanganywe na wafungwa wengine kwani wafungwa wote wanastahili kupewa haki sawa.
Meek kwa sasa anaweza kufanya kazi mojawapo kati ya mbili ambazo atachagua kufanya akiwa gerezani na kipato atakachopata atachangia 19 cents kwenye mfuko wa gereza lakini pia anaweza kufanya kazi nyingine ikiwemo kupika, kufanya usafi na kusoma vitabu.

Sasa unaweza Kudownload Teknomovies App kwa wewe mtumiaji wa Android cha kufanya nenda Google Playstore Udownload ili uwe wa kwanza kupata mastori makali.


No comments:

Post a Comment

Pages