Ukweli Kuhusu Scenes Za Mapenzi,Je ni Ukweli Ama Danganya Toto#Uchambuzi - teknomovies
Ukweli Kuhusu Scenes Za Mapenzi,Je ni Ukweli Ama Danganya Toto#Uchambuzi

Ukweli Kuhusu Scenes Za Mapenzi,Je ni Ukweli Ama Danganya Toto#Uchambuzi

Share This
Moja ya suala ambalo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara ni kuhusu uchezaji wa scene za ngono kuwa ni kweli huwa zinafanyika au huwa ni maigizo tu.
Jambo moja ambalo watu wengi inabidi wakumbuke ni kuwa Filamu ni maigizo,Hivyo kwa asilimia kubwa kila jambo linalofanyika ni maigizo lakini pengine watu watakuwa wanamashaka na hilo hasa kutokana na tabia pengine za wazungu kuonekana kuwa na vichaa na pia uhalisia mkubwa wanaounesha katika filamu zao.

Kumbuka kuwa,katika maisha ya kawaida kuna vitu vingi vya kuchezeana lakini si pale kati bhana,Sababu waigizaji wengine wanakuwa wameolewa na kuoa hivyo kuonjeshana zile sehemu kwa sababu ya fedha si jambo la kirahisi kama unavyofikiria.

SOMA PIA:KIFO CHA BRUCE LEE

Baadhi ya waandaaji wanakiri kuwa katika scenes ambazo ni ngumu sana kuziandaa basi mojawapo ni Scene za ngono.

Kabla ya kufanyika kwa Scenes hizo unaambiwa kwanza waigizaji huwa wanafundishwa baadhi ya mbinu na kuna muda mwingine wanaladhimika kutumia vilevi ili kuifanya miili ionekane kingono zaidi na mara kwa mara kabla Scenes hizo hazijaanza kuchukuliwa Push Ups pia huwa zinahusika ili kuweka misuli kuwa fresh kwa tendo hilo la kuigiza.
Mwandishi na pia muongozaji wa Filamu maarufu,Sarah Treem anaefahamika kwa kazi kama House of Cards na pia The Affair anasema kwanza kuna utofauti mkubwa sana kwa namna ambavyo Sex Scenes zinaandikwa na kuongozwa.

Anaongeza kuwa ,Siku ya Kushoot huwa kunakuwa na mabadiliko mengi sana sababu kuu ni scene ambazo zinahitaji umakini mkubwa na ni muhimu sana hasa kwa waigizaji.

Judd Apatow ambae ni muongozaji na pia mwandishi mkubwa wa filamu akifahamika hasa kwa kazi kama Get Him To The Greek,Zookeeper,This Is 40,Superbad N.K anafunguka kuwa Huwa anapenda kuchukua picha nyingi sana kwa kila angle siku ya kushoot scenes hizo lakini mwisho wa siku zote huwa zinaachwa na kutumika chache sana. 

SOMA PIA:MAKUNDI MAWILI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI

Kwa tafsiri hiyo,Scene za mapenzi hizo zinachukua muda mrefu sana kuzirekodi na pia angle nyingi hutumika kuchukua scene hizo lakini ni kiasi kidogo tu hutumika katika filamu ambayo watu huja kutazama.
Lakini kumbuka vitu kama mabusu na romance huwa ni kweli lakini mara nyingi huwa ni tofauti kwa waigizaji wenyewe ambao wanakiri kuzichukia sana hizo scenes ambazo kwao wanasema huwa hazina hisia kama watu wanavyofikiria.
Lakini katika kushoot huwa inategemeana na mkataba ambao waigizaji wanakuwa wameingia hasa katika suala la kuonesha miili yao.
Sarah Treem anafunguka zaidi,Kabla ya kushoot kwa kawaida waigizaji wanakuwa na vitu vyao vya umuhimu ambavyo hawapendi kuonesha na sisi waandaaji huwa tunaheshimu hilo.

Anaongeza zaidi kuwa mara nyingine tunajaribu kushoot scene hizo na kumfanya mtazamaji kutokugundua kama tulikuwa kuna vitu na ndo hapo unaona kwa mfano scene inachukuliwa kwa kubana zaidi na kuonesha sura tu za waigizaji.

SOMA PIA:ROSA REE UKWELI WOTE HUU KUMUHUSU YEYE HUU HAPA

Lakini pamoja na hilo waigizaji huwa kuna muda wanavaa vifaa maalumu ili kuficha sehemu zao muhimu mfano katika filamu ya Fifty Shades Of Grey Jamie Dornan aliweka kitu katika uume wake na pia Dakota aliweka kifaa maalumu sehemu zake za siri na pia mwili mzima.
Dakota Johanson
Baadhi ya vifaa ni kama:
Merkin
fresh toned Undergarments
Pasties
Dakota Johnson anasema kushoot scenes hizo huwa kunakuwa na presha kubwa sana hasa kutokana na kuzungukwa na mitaa mingi na pia huwa sio za utulivu hata kidogo kama watu wanavyofikiria.
Mila Kunis
Mila Kunis anasema ni vigumu sana kucheza sex scenes sababu ni muda gani mtamaliza haijalishi na kama ni rafiki,mwanaume au mwanamke haijalishi na pia unakuta upo na watu 100 zaidi ambao ni waandaaji wanakumulika na kila mara kuwarekebisha kwamba make hivi na vile kwahiyo hata huwa hazipo poa kama watu wanavyofikiri.

Kwa maana hiyo Scene nyingi za mapenzi si za kweli kama wengi wanavyofikiri japo miili yao kuwa uchi na mambo mengine huwa ni kweli lakini sio kupitishana vikojoleo hapo ndo huwa suala gumu kidogo.

SOMA PIA:MFAHAMU SCARLETT JOHANSON

Japo mara kadhaa imeripotiwa baadhi ya scenes watu walibanjuana ukweli,lakini jambo muhimu la kujua kila unachoona katika filamu asilimia kubwa ni Maigizo na hakuna ukweli wowote.

Unaweza Kutazama Video Fupi Hapo Chini na Tazama Namna Wanavyofanya katika kushoot Scenes Hizo

               
Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.

Sources:Newyorktimes.com,The Independent na vyanzo vingine pamoja na picha kwa msaada wa mtandao.

Pages