Nini Chanzo Cha Kifo Cha Bruce Lee#Fahamu - teknomovies
Nini Chanzo Cha Kifo Cha Bruce Lee#Fahamu

Nini Chanzo Cha Kifo Cha Bruce Lee#Fahamu

Share This
 
 "Hata Kama Nikifa Kesho,Siwezi Kuumia Maana Nishafanya Vingi Na Kupata Vitu Vyote Nilivyokua Nikitamani Kua Navyo Ko Sitegemei Mengi Mapya Saana"

Ni Moja Ya Jibu LA Star Jay Z Alipoulizwa Swali Na Mtangazaji Hiyo Ilikua Ni Baada Ya Kupata Mtoto Wake Wa Kwanza Na Mke Wake Beyonce.

  Ilikua Ni May 10th Mwaka 1973 Bruce Akiwa Katika Studio Za Golden Harvest Studios Ilikua Ni Kipindi Ambacho Alikua Akitayarisha Mzigo Wake "Enter The Dragon" Sasa Baada Ya Kazi Nzito Ulifika Muda Wa Mapumziko Kidogo Ambapo Bruce Alienda Toilet Kufanya Alichokusudia.

Alikaa Huko Kwa Takribani Dakika 20 Kitu Kilichowastua Baadhi Ya Wenzake Ambapo Mmoja Akaamua Kwenda Kumchungulia Huko Toilet Vipi Tena Kulikoni?

Mwenzake Alipomfuata Toilet Alimkuta Bruce Akiwa Kainama Chini Huku Akiwa Anapapasa Papasa Chini , Mwenzake Alipomuuliza Kuna Tatizo Gani?

Bruce Akamwambia Kua Alikua Anatafuta Miwani Yake,Lakini Hakua Katika Hali Sawa.

 Wakiwa wanarudi Studio Ghafla Bruce Alianguka Huku Akiwa anatetemeka Na Mapovu Yakimtoka Mdomoni.

Kwa Haraka Wenzake Wakamstua Mkuu Wa Studio Bwana Raymond Chow,Ambapo Badala Ya Kupiga 911 Yeye Akampigia Doctor Wake Anayefahamika Kwa Jina LA Doctor Langford Ambapo Baada Ya Kuelezwa Tukio Hilo, Akaamuru Bruce Apelekwe Hospitali.

Kutokana Na Hali Ya Bruce Kuonekana Kua Kama Ana Kifafa Hivi, Doctor Langford Alimwita Neurologist ( Mtaalamu Wa Magonjwa Ya Mashambulizi Ya Ubongo, MTi Wa Mgongo Na Mifumo Mingine Ya Neva)

 Doctor Wu Ndo Jina Alifahamika Doctor Huyo Ambapo Baada Ya Kufanya Check Up Ya Mwili Wa Bruce Majibu Yalikuja Ambapo Bruce Alionekana Kua Na Uvimbe Katika Ubongo Wake Ambapo Alipewa Dawa Ikifahamika Kwa Jina LA Mannitol Ili Kupunguza Uvimbe Huo.

Pia Bruce Alikutwa Kua Na Kiasi Fulani Cha Hashish Ndani Ya Tumbo Lake.

Baada ya Tukio Hilo , Mke Wa Bruce Alipewa Taarifa Ya Mumewe Ambapo Alifika Baada Ya Nusu SAA,Na Baada Ya SAA Moja Baadae Bruce Alipata Ufahamu Na Alianza Kuongea Kidogo Ila Maneno Yalikua Hayasikiki.

Siku Iliyofuata Doctor Langford Alimuuliza Bruce Kuhusu Swala LA Utumiaji Wa Madawa,Ambapo Bruce Alikubali Kua Anatumia Madawa Aina Ya Hashish Inayotoka Nepal.

Bruce lee pamoja na familia yake.
Doctor Alimuonya Kuhusu Madawa Hayo ,Na LA Zaidi Alimwambia Kua Madawa Hayo Kutoka Nepal Ni Hatari Sana Mana Ni Kitu Pure Halisi,Lakini Bruce Hakusikia.
 Bruce Baada Ya Kuonywa,Hakusikia Hivyo Aliendelea Na Matumizi Ya Madawa Mpaka Tarehe 25th May Ambapo Alisafiri Kwenda Marekani Ili Kwenda Kucheki Afya Yake Vizuri Zaidi Ambapo Alipopimwa Kwanza Uzito Wake Ulikua Umeshuka Sana Sana Akiwa Na 57Kg,Lakini Doctor Alimwambia Yu Vizuri.

Baadae Alienda Tena Kwa Neurologist Ambapo Baada Ya Kuchekiwa Afya, Alionekana Kua Na Kifafa Lakini Chanzo Cha Kifafa Hakikufahamika,Lakini Nae Doctor Alimwambia Kua Yupo Katika Hali nzuri.

Tarehe 20 Mwezi July  Ni siku ambayo Bruce Ilitakiwa awe na Mke Wake Linda Maana Ilikua Ni Muda Kidogo Hawajaonana Lakini Kabla Ya Kuonana Linda Alikua Na Appointment Na Marafiki Zake Nae Bruce Alikua na Kikao Na Raymond Chow Ambapo Bruce Na Chow Walikua Wakiandaa Script Ya Movie Mpya Iliyopewa Jina LA GAME OF DEATH

Walionana SAA nane Mchana na Wakapiga Kazi Mpaka SAA Kumi Jioni Ambapo Walitakiwa waende Kuonana na MTU mmoja aliefahamika kwa jina LA GEORGE LAZENBY katika Hotel Ya Miamar, Lakini kabla Ya kwenda huko waliamua kwanza wapitie kwa mwana mama Betty Ting Pei Lengo Likiwa Kumuomba Kucheza Katika Movie Hiyo.

Walipofika Huko Wakati Maongezi Yakiendelea Kwanza Ray Aliwaacha Bruce Na Betty Ili Kwenda Kuonana na George Ila Akitegemea Kua Bruce Nae Atakuja Baada Ya Kumaliza Mpango Mzima.

Bruce Akiwa na Betty Ghafla Alianza Kulalamika Kichwa Ambapo Betty Alimpatia Dawa zake za kutuliza maumivu.

Lakini hali ilizidi Kua mbaya zaidi Ambapo Bruce Alienda kupumzika Kwenye Kitanda cha Betty.

Hiyo ilikua kama mida ya SAA tatu usiku,Baadae Ray Alimpigia Simu Betty Kua Mbona Hajawaona kwa meeting? Betty akamjibu Tatizo Huku Bruce Najaribu Kumuasha Lakini Haitiki.

Ray Akamwambia anakuja , Nusu SAA Akawa Amefika Na Kweli Akajaribu Kumuamsha Lakini Hali Ilikua Tete Ambapo Ikabidi Akimbizwe Hospital Haraka Hiyo Ilikua Mida Ya SAA NNE Usiku.

Madaktari Walifanya Kila Linalowezekana Kuokoa Maisha Ya Bruce Lakini Siku Ikifika Imefika Tu.

Ray Alimpiga Linda Simu Kumwambia Hali Ilivyo Na Linda Bila Kuchelewa Alifika Hospital Hiyo Ya Queen Elizabeth.

SAA Tano Usiku,Ndipo Taarifa Za Kushtushwa Zikatolewa Kua Bruce Hatunae Tena Katika Dunia Hii.

siku ya mazishi ya Bruce lee watu wakiwa Barabarani.
Tarehe 25 July Maombolezo Yalifanyika Huko Hongkong Ambapo Zaidi Ya Watu 25,000 Walihudhuria Kumuaga Kipenzi Chao. ( Ukitaka Uwauzi watu Wa Hong Kong Mtukane Bruce).

Baada ya Hapo Mwili Wa Bruce Ilitakiwa Kusafirishwa Kwenda Marekani Kwaajili Ya Maziko Mana Ndo Sehemu Alikozaliwa Lakini Kabla Mwili wake Haujasafirishwa Kwenda Huko Mke Wake Aliongea Maneno Haya Kwa Huzuni Kubwa Namnukuu...
"However the investigation is not yet closed to the death of my husband, I wish the press and the people of Hong Kong would stop speculating over the cause of death of my husband.
 I haven’t any suspicions than that Bruce has died naturally. I don’t blame myself or anybody else for that matter for his death. Our destination is unpredictable. The only irrelevant thing here is that Bruce has died and he will never return.
He lives on in our memories and through his films. Please remember Bruce because of his talent, his art and the magic he gave us all.
For those of you who knew him better, his words andthoughts will always be with us and will have influence on us for the rest of our lives.
 I know, that the people of Hong Kong loved Bruce and are very proud of him because of what he has achieved, he had managed to get worldwide attention for Hong Kong. That’s why I’m begging you to please leave him to rest in peace and do not disturb his soul. These are my personal feelings and wishes and thatof my closest friends. I would appreciate it if you would listen to me and respect our wishes"

Tafsiri " Ingawa Bado Uchunguzi Unaendelea Wa Kifo Cha Mume Wangu,Nategemea vyombo vya Habari Na Watu Pia Wataacha Kuzungumzia Kifo Cha Mme Wangu. Sina MTU yeyote Wa Kumlaumu zaidi najua Bruce Kafariki Kawaida Tu.Sijilaumu Mimi Au MTU Yeyote Kwa Kifo Chake Inatakiwa Tujue Kua Mwisho wetu Hautabiriki.
Kitu Tofauti Hapa Ni Kua Bruce Amekufa Na Hatarudi Tena.Ataendelea Kuwepo Katika Kumbukumbu Zetu Kupitia Filamu zake Na Nawaombeni Jamani Tumkumbuke Bruce Kutokana Na Kipaji Chake,Sana'a Yake Na Maajabu Yake Aliyotuachia.
Kwa Wote Mliomjua Vizuri,Maneno yake Na Mitindo Yake Itabaki Miongoni Mwetu Na Itabaki Kama Mchango Katika Maisha Yetu Daima.
Najua Ni Kwa Jinsi Gani Watu Wa Hong Kong Mlimpenda Bruce Na Mlikua Mkijivunia Kua nae Yote Kutokana Na Mafanikio Yake Maana Aliweza Kuyaelekeza Macho Ya Dunia Kua Hapa Hong Kong,Na Ndomana Nawasihi Tumuache Apumzike Kwa Amani Na Tusiisumbue Roho Yake.
Hizi ni Hisia zangu na za Marafiki Zangu Wa Karibu na Nitafurahi Sana Kama Mtasikiliza Na Kuheshimu Matarajio Yangu
" Alimaliza Linda.


Tarehe 30 July Mwaka 1973 Alizikwa Huko Settle,Washington Na Marafiki Zake Wa Karibu Takribani Watano.

Tarehe 24 Mwezi September Taarifa Ya Kuhusu Kifo Cha Bruce Lee Ilitolewa Ambapo Majibu Ya Uchunguzi Yalikua Ni Kama Ifuatavyo.....

Cha Kwanza Ukitoa Matumizi Ya Madawa Bruce Lee Mwili Wake Wanasema Ulikua Uko So Hyper Sensitive Kwa Baadhi Ya Madawa Ambapo Kuna Madawa Kama Equagesic,Doloxene na Dilantin Hayo Yote Ni Dawa Za Kutuliza Maumivu Ambazo Alikua Akizitumia Katika Miaka Ya 70 Katika Kutuliza Maumivu Alipoumia Kipindi Cha Mazoezi.

Sababu Nyingine Bruce Lee Mwili Wake Ulikua Na Kiwango Kidogo Sana Cha Fati Yani Asilimia 1% Tu

Sababu Nyingine Ni Bruce Lee Alikua Akiutumikisha Mwili Kwa Kiasi Kikubwa Yani Alikua Anapenda Kufanya Kila Kitu Yeye Sijui Actor, Director, Script Na Choregrapher.

Pia Tatizo Lingine Ni Kupungua Kwa Uzito Wa Mwendokasi Ambapo Alipungua Toka Uzito Wa 70 Kilo Kwenda mpaka 60 Kumi Alipoteza Kwa Haraka Sana.

Na Zaidi Watu Wa Mwisho Mwisho Kuonana Nae Wanasema Jamaa Alikua Anaonekana Kuchoka Hivi Afu Pia Alikua Ana Sahau Sahau Pia Alikua Na Hasira Hasira Hivi Na Alikua Kakonda Kweli Yani.
Kabuli la Bruce lee pamoja na mtoto wake Brandon










Pages