Ukiachana na miondoko yote hiyo Hip hop imejizolea masabiki wengi sana duniani kwa namna ya uimbaji wake wa kufoka foka na utunzi wa mashairi yanayopangiliwa kwa mfumo wa vina. Style ya uimbaji wake imepelekea kujengeka kwa makundi ambayo yanaingia kwenye uhasama wa kikazi lakini pia usishangae kuona uhasama huo unaingia hadi kwenye maisha binafsi hali inayopelekea kutokea kwa vurugu zinazopelekea hadi vifo kwa baadhi ya wasanii.
Ukizungumzia makundi makuu ya hip hop yaliyoingia
kwenye uhasama (Pengine hadi leo upo) ni makundi mawili kutoka Marekani ambayo
ni East Coast na West Coast Rivalry, lakini kabla ya kuyajua makundi haya
kwanza tujue chimbuko la Hip Hop.
Harakati za muziki wa Hip Hop zilianza miaka ya
1970’s katika mitaa ya Bronx eneo la South Bronx lililopo New York City na
miongoni mwa waasisi wake ni DJ’s kutoka Jamaica Kool Herc, Grandmaster Flash
na Afrika Bambaataa. Eneo la New York City lilikuwa maarufu sana miaka ya 1980’s
katika Nyanja ya muziki wa Hip Hop huku mastar kadhaa kama Run-DMC, LL Cool J,
KRS- One, Doug E. Fresh, Rakim, Big Daddy Kane na wengine wengi wakiufanya mji
huo uwe juu kwenye miondoko ya Hip Hop.
DJ Kool Herc |
Hip Hop iliteka hisia za wasanii wengi tu kuanzia
America na hata Africa kwa namna ya utungaji wake wa mashairi na uwasilishaji
wake kwa mlaji (shabiki). Kutokana na kuteka hisia kwa wapenzi wa muziki baadhi
ya record label zikaelekeza rada zake kwenye mziki huo kwani ulikuwa ukiuza
sana sokoni.
KRS-One |
Baada ya New York City kutambulisha wasanii wake
kwenye ramani ya hip hop, mwaka 1986 Ice-T kutoka mtaa wa Crenshaw uliopo Los
Angeles ambapo ni West Side akaachia ngoma yake ya kwanza “6 in the morning” na
hivyo ikaanza kukosolewa vikali na upande wa pili (East side).
SOMA PIA:MAKUNDI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI 2
SOMA PIA:MAKUNDI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI 2
Baada ya kuachia ngoma yake Ice-T akiwa na rafiki
zake Jerry Heller na Eazy-E wakaunda record label iliyojulikana kwa jina la
Ruthless Record. Baadae kidogo wakatoa albam ya “Panic Zone” ambapo kundi lao
walilipa jina la N.W.A (Niggaz With Attitude) humo ndani alikuwepo Arabic Prince, Eazy – E
na mkali Ice Cube. Kutokana na masuala ya kifedha kundi hili lilikuja kuvunjika
baadae na Eazy- E akabaki kuwa meneja wa record label ya Ruthless Record.
Dr Dre Baada ya muda record label zikaanza kuenea maeneo ya West side ambapo Dr Dre nae akaanzisha record label ya Death Row Record akiwa na Suge Knight. |
Itaendelea..........