WANASEMA ndio sehemu ambayo burudani nzuri hua inatoka kwa
sana, lakini pia ndio sehemu ambayo inaongoza kwa Drama nyingi sana kuanzia
skendo za hapa na pale na mambo mengine mengi.
Ni Wcb,ambapo wakati ishu ya Harmonize na Wolper ikiwa bado haijapoa
huku nako Rais wao Diamond Platnumz ishu bado inazidi kuwa tat asana.
Hakuna asiejua suala la uwepo wa tetesi juu ya mgogoro kati
yake na mwenza wake Zari ambapo jana katika picha aliyoweka Instagaram Diamond,
Mwenza wake huyo Zari aliweka maoni yake kwa kuweka emoji ya kuonesha kidole
cha kati....Tazama Hapa Chini.
Pengine unaweza hisi labda alikosea lakini alifanya hivyo mara
mbili hiyo kuonesha msisitizo zaidi kwa kitu alicho komenti.
Uwepo wa mgogoro baina yao ulianza kipindi ambacho inasemekana
Diamond alitembea na mwanadada Hamisa Mobetto ambae alipata ujauzito unaodaiwa
kuwa ni wa Diamond.
Ishu ikazidi kuwa tamu zaidi baada ya Mobetto kujifungua na
kuamua kumpa mtoto jina lake AbdulNassib ambalo ndio jina halisi la Diamond.
Hamisa Mobetto |
Pia mwanzoni ilibainika kuwa mahusiano ya Mama Diamond na Zari
si mazuri na hivyo kuzidi kuhatarisha zaidi penzi la hao watu wawili ambalo
limeweza kudumu kwa kipindi kirefu zaidi .
Yote na yote filamu bado inaendelea acha tuendelee
kuisikilizia.
No comments:
Post a Comment