USIYOYAJUA KUHUSU FILAMU YA TITANIC - teknomovies
USIYOYAJUA KUHUSU FILAMU YA TITANIC

USIYOYAJUA KUHUSU FILAMU YA TITANIC

Share This
Kwa wapenzi wa Filamu za nje ni wachache ambao utawakuta hawajawahi kutazama hii filamu iliyojizolea umaarufu mkubwa hasa kutokana na ubora wake.
Ukiitizama hata leo, unaweza usiamini kua ni filamu iliyotengenezwa mwaka 1997 kutokana na ubora wake na mpaka sasa imeweza kuweka rekodi kadhaa kama kushika nafasi ya pili katika filamu zilizo uza zaidi kwa muda wote ikiwa imeuza Dola bilioni $2.1.
Licha ya mafanikio mbalimbali ,Filamu hii imejaa vitu vingi ambavyo watu wengi hawavitambui, na vitu hivyo vitakuacha midomo wazi na kubaki kutafakari kwa makini ubora wa watu hawa katika uandaaji wa Filamu zao, Anza Sasa;

    Michoro Ya Jack sio Yeye aliyekua anachora, ni Mtu mwingine.
Mojawapo ya kivutio kizuri katika filamu hii ni michoro ya Jack, hususani pale alipokua akimchora Rose Jambo ambalo kuna watu wanaamini kwamba Jack alikua ana kipaji kweli cha uchoraji. Lakini hali halisi michoro yoote uliyoona ambayo Jack alikua nayo na Hata pale alipokua akimchora Rose, sio yeye aliyekua Anachora bali ni Muongozaji wa Filamu Hiyo James Cameroon ambaye ndiye aliyechora kila mchoro na hata pale alipokua anamchora Rose, aliyekua anafanya hicho kitendo ni James na si Jack kama iliyoonekana. James anatumia mkono wa kushoto na Jack ni mkono wa kulia,Hivyo kilichofanyika ni kuchezesha vipande hivyo  na walitumia vioo maalumu ili aonekane ni Jack aliyekua anafanya hicho kitendo.

      Wakati meli imeanza kuzama na maji yameanza kujaa ndani ya meli,

 kuna sehemu ilionesha wazee wawili ambao walikua mke na mume ambao walikua wamelala Kitandani katika Chumba na katika Tukio halisi la kuzama kwa meli ndivyo ilivyotokea ambapo wazee Hao walifahamika kwa majina ya Ida na Isidor Strauss wakazi wa Mji wa New York ambao walifariki Katika ajali hiyo mwaka 1912. Bibi kizee Ida inasemekana kua alipewa nafasi katika boti maalumu za uokozi  lakini alikataa sababu alitaka kubaki na Mume wake anakaliliwa kua aliongea maneno haya “ As we lived together, So we shall Die Together “ ( Kwa jinsi Tulivyoishi
pamoja,Ndivyo Tutavyokufa pamoja).
Na kuna kipande katika filamu  ilishutiwa kuonesha jambo hilo lakini ilifutwa mwishoni wakati filamu ikimaliziwa kufanyiwa editing, kama wasingeitoa basi tungefaidi uhondo huo.

      Kate winslet ( Rose) alikataa kuvaa Wetsuit
( Nguo maalumu kwaajili ya uogeleaji) wakati wa Kushuti filamu jambo lililopelekea kuugua Pneumonia na ilibaki kidogo kuacha Kushuti Filamu hiyo sababu ya ugonjwa ila Shukrani kwa watoa huduma waliofanikisha kuweza kuturudishia kipaji hichi.

      Filamu iligharimu pesa nyingi sana kuzidi hata matengenezo ya meli yenyewe. Bajeti ya filamu iliyotumika ilikua ni Dola milioni $200 na bajeti nzima iliyotumika kutengeneza meli yenyewe iliyozama ilikua ni Dola milioni $7.5 kwa miaka hiyo ambapo kwa sasa ingekua kwenye Dola milioni $150 .

     Kama sio Kate Winslet (Rose) basi ungemuona Madonna
maana nae alikua mmoja ya watu waliokua wanaangaliwa kucheza nafasi hiyo na alifanya usaili, lakini hakupita sababu waandaaji walimuona kama Umri kwake ulikua mkubwa sana kuliko uhusika wenyewe wa Rose Je ushajiuliza ingekuaje kama ingekua sura Ni tofauti na Kate?

     Ilikua ni Filamu ya Kumi Kwa James Cameroon kuongoza,
na Filamu pekee ya kwanza Kutoka kwake ambayo haikuingiza maneno yoyote au kuhusisha mambo ya Nuclear, Filamu zake zilizopita dhamira ya mambo ya Nuclear ilikuepo kama Terminators, Dark Angel Nakadhalika.

     Groria Stuart aliyecheza kama Bibi kizee Rose,
anashikilia rekodi ya kua mtu mzee zaidi kuweza kuchaguliwa katika moja ya vipengele katika tuzo za Oscar ambapo alichagulia katika kipengele cha Best supporting actress akiwa na miaka 87 lakini katika filamu uhusika wake uliwekwa akiwa na miaka 100. Kilichofanyika zaidi kumuweka mzee zaidi, nae alifanyiwa make up ya nguvu. Pia Groria ndiye alikua mtu pekee aliyecheza filamu hiyo ambapo pia wakati Meli halisi inazama alikuwa hai. Grory alifariki mwaka 2010 akiwa na miaka 100 sawa na miaka ya uhusika wa filamu kwa matatizo ya kansa ya Mapafu.


    Filamu inashikilia rekodi ya kua Filamu ya kwanza kuachiwa katika mfumo wa video wakati bado ikiwa inaoneshwa katika Sinema mbalimbali yote ilitokana na umaarufu wake. Na pia filamu hii ilidumu sana katika Majumba ya sinema mengi sana kuzidi kawaida, ambapo katika nchi nyingi kwa zaidi ya miezi 9 bado ilikua inaoneshwa.

     Kabla ya kupewa jina la Titanic,filamu ilipewa jina la Planet Ice baadae ndo ikabadilishwa.

 James Cameroon hakutaka kabisa kuhusisha  nyimbo (soundtracks)  
katika filamu hiyo lakini moja ya waandaji pia Mr James Horner alimchukua Celine Dion pamoja wakatengeneza wimbo “ my heart will go on”pale alipomsikilizisha James,alibadiri upepo wake na akakubali kuutumia wimbo huo kama wimbo maalumu katika filamu hiyo lakini jua hili, Celine anasema yeye hakuupenda huo wimbo na chaajabu ni Demo tu ndiyo iliyotumika kumshawishi James.

  Kuna sehemu Jack alikua anasema  kua yeye Amewahi  fanya kazi ya uvuvi
katika ziwa alilotaja la Wissota. Lakini ukweli ni kua  Ziwa hilo kwa mwaka 1912 halikuepo ,sababu ni ziwa ambalo lilitokea kutokana na Shughuli za kibinadamu na  lilitokea rasmi mwaka 1917.

  Wakati amemaliza kuandaa script James Cameroon ndipo alipojua kua kumbe Kulikua na mtu ambae alifariki nae katika ajali hiyo aliitwa J.Dawson
sema yeye alifahamika kama Joseph. ( Wahusika wakuu waliitwa Jack Dawson na Rose Dewitt katika Filamu) Kaburi la Jamaa huyo mpaka sasa huwa linatembelewa na watalii wengi sana

  Studio ilimtaka Matthew McConaughey kucheza kama Jack Dawson lakini James alisisitiza kumtaka Leornado Di Caprio ndiye acheze nafasi hiyo. Hapa napo vipi kama angecheza mtu tofauti na Leo je unazani bado ingebamba zaidi.

  Katika scene ambayo Rose alikua katika bodi ya mbao na jack akiwa kashikilia, utafiti ulifanywa na ilionesha kua bodi hilo lilikua na uwezo wa kuwabeba wote wawili kwa saa nzima  mpaka
walipokuja kuwaokoa. Mjadala ulianzia kwa mashabiki wengi waliojikuta wakilaumu kwanini Jack alifariki wakati alikua ana uwezo wa kupanda katika bodi hilo. Chaneli ya Discovery ilifanya utafiti huo kisayansi na jibu ilikua ni ukweli kabisa.

  Picha za chini zikionesha Meli ya Titanic iliyozama ni Picha halisi kabisa za meli iliyozama mwaka 1912.
James alitaka kuonesha uhalisia zaidi hivyo aliita timu maalumu Russian Research vehicle na Nyambizi 2 ambazo kupata picha toka meli hiyo walishuka chini kwa urefu wa 12,500 na kuna habari ambayo imeeleza kua Meli ya Titanic kufikia mwaka 2030 inaweza kutoweka kabisa baharini.

 Filamu nzima iliigizwa katika Bwawa la Kuogelea ( swimming pool) na si katika bahari kama wengi walivyoona katika filamu.

James aliamua kutengeneza mfano wa meli ya Titanic

lakini kwa upande mmoja tu na baada ya Filamu kumalizika vyuma na vifaa vingine vilipigwa bei kama vyuma chakavu.

  Kuwashawishi kampuni ya 20th century Fox Cameroon aliwaambia kua filamu hiyo ni kama Romeo and Juliet
lakini ambayo imetokea katika Meli hivyo baada Kampuni kusikia haikutaka kumpoteza Cameroon wakakubali kuifadhili Filamu.

  Bibi kizee Rose katika Filamu alionekana akiwa ana miliki mbwa Jamii inayofahamika ya Pomeranian.
Katika ajali halisi moja kati ya mbwa watatu ndio pekee walioweza kupatikana wakiwa hai, na katika filamu kuna vipande ambavyo vilichukuliwa kuonesha tukio hilo lakini James alitoa vipande hivyo

 Nafasi ya Captain Adam Smith alitakiwa kucheza mtaalamu Roberto De Niro
lakini alishindwa kuchukua nafasi hiyo kutokana na Ugonjwa uliokua ukimsumbua kwa kipindi hicho hivyo nafasi akapewa mtu mwingine.

Vyanzo:Buzzfeed.com na Mitandao Mingine

DOWNLOAD HERE TITANIC MOVIE

Unaweza Kutazama Pia Kwa Kubonyeza Hapo Chini ,Tazama Behind The Scene Katika Swimming Pool

            

Pages