Mambo Usiyofahamu Kutoka Kwa Ndege Tai (Eagle)#Uchambuzi - teknomovies
Mambo Usiyofahamu Kutoka Kwa Ndege Tai (Eagle)#Uchambuzi

Mambo Usiyofahamu Kutoka Kwa Ndege Tai (Eagle)#Uchambuzi

Share This
Ndege huyu ana kila aina ya sifa ambazo hujitokeza kwa ndege wenzie, pia ni ndege ambaye jina lake linajitokeza hata katika vitabu vya dini, kwa asili ni ndege mkorofi sana, si kwa wanyama wengine anaopenda kuwabughuzi kwa kuwaparua kwa makucha yake, bali hata ndege wenzie huionja shubiri yake, achilia mbali mchezo wake wa kunyang'anya chakula kwa binadamu. 


Ni ndege mwenye nguvu sana kiasi cha kufanya baadhi ya Mataifa makubwa kumtumia kama mnyama wa Taifa, kwa Afrika Egypt wamempa heshima hiyo, na Taifa la marekani wanafanya hivyo pia.

Pamoja na sifa hiyo pia Tai ni ndege mwenye mbio sana, ukimtoa ndege kozi ni yeye ambaye hufuata kwa kukimbia, zipo aina nyingi sana za Tai na kila mmoja wao hubeba sifa yake ya upekee, wapo ambao hukimbia sana, wapo ambao ni wakatili sana, wapo wapole na wengine wengi wenye sifa kem kem.

SOMA PIA:WANAOTUMIA SIMU NJIANI KUKAMATWA MAREKANI

Unapomuona jicho lake huwa na rangi nyeusi iliyotawala sana, mdomo wake umechongoka, miguu yenye nguvu na kucha kali, mbawa zake ni kubwa sana na ndio humfanya aonekane na kimo kikubwa zaidi pamoja kwamba mwili wake si mkubwa sana, uzito wake hucheza kati ya kg 4 mpaka 8, miaka yake ya kuishi huwa ni zaidi ya 25, na chakula chake kikuu ni nyama, huweza kula mizoga, nyoka wakubwa, wanyama wadogo nk. 

Ni ndege mwenye sauti nzuri sana awapo angani, inapendeza kutumika kama muito wa simu (ringtone),kwa watengenezaji wa filamu pia sauti yake inapendeza ikitumiwa katika upambaji wa matukio au mwanzo wa filamu, anapotoa sauti yake hiyo pamoja na uzuri wake kwa ndege wenzie huwa ni hofu, mwewe, bundi, kozi hujihadhari kwa kukaa mbali, na sauti yao hiyo hubadirika kutokana na mawasiliano wanayofanya baina yao.


SOMA PIA:PAKUA ALBAMU MPYA YA SAM SMITH

Ndege Tai anaogopeka sana, kiasi kwamba kimvuli chake kionekanapo tuu, wanyama wadogo hukimbia hovyo, na wakubwa wakitafuta njia za kupambana naye.

SIFA ZAKE ZA KIPEKEE

1. Ni ndege muwindaji sana, kama walivyo wanyama wengine wala nyama mfano simba, chui nk.


2. Mashambulizi yake ni ya kushitukiza sana, akiwa angani hufyatuka kama mwewe aibapo kifaranga, lakini kama atakuwa anawinda kiumbe ambacho kukabiliana nacho si jambo jepesi utamuona akitizama kwa maringo juu ya mti na akifuatilia hatua za kiumbe huyo mdogo mdogo.


3. Pamoja kwamba jicho lake ni dogo lakini uwezo wake wa kuona ni mkubwa sana, kama upo nje tizama juu macho yako yanapoishia kuona yeye huona mara nne zaidi.


4. Tai hawezi kuwinda mwanadamu, lakini akitambua binadamu ni mgonjwa, dhaifu, goigoi atahangaika na wewe tuu.


5. Huweza kubeba viumbe wazito na hufanya hivyo kwa sababu zifuatazo mosi kuhofia usalama wake anaponyakua windo katika jamii ya wanyama hao, pili hubeba kisha huchia kutoka juu lengo likiwa ni kupasua na aweze kula kwa urahisi.


6. Ubabe wake humfanya naye kujenga ngome imara sana, yaani viota ambavyo hujenga vikubwa na huzungusha kwa miiba ili tuu kuzuia nyoka wasiweze kuwafanya wanaye au mayai yao kama mlo.


7. Bibilia inasema kupitia mithali ya kwamba mwendo wa tai ni wa kustaajabisha na kushangaza, kama hilo lilinakutatiza kufahamu nakujuza ya kwamba awapo juu, tai huweza kuganda kwa muda kidogo, na anaweza kuendelea na safari pasina kupiga mbawa zake, akiwa katika mwendo mdogo.

Tai Wakijamiiana

8. Tai ni waaminifu katika mapenzi, huishi kwa kusaidiana na kuaminiana sana, aina ya Tai wabaya huwezi kuta dume akitafuta jike mwingine au jike akihangaika na dume mwingine, anapotoka mapenzi yake hubakisha kwa mwenza wake, na mwenza wake asipomuona mwenzie kwa siku mbili hupata hisia ya kwamba huenda mwenzie kauwawa, hapo huondoka na kutafuta mwenza mpyaa.
Kifaranga cha Tai

9. Tai hurudia viota vyao, kila baada ya muda flani wanapotaka kutaga, hufanya ukarabati kidogo tuu.
10. Wakiwa katika kundi wakakuweka kati binadamu dakika 20 nyingi minofu yote watakuwa washamaliza.


Je ungependa kuwaona ndege hawa, Tanzania tunao katika mbuga zetu, Kilimanjaro, udzungwa pia Serengeti ukifika huko utafurahi na roho yako, achana na uzushi ya kwamba Tai anaweza beba binadamu labda umkaribishe wewe mwilini mwako endapo utakuwa una vinono unakula na yeye akakuona utakula nae sahani moja.....


Tazama hapa chini video ya Ndege Huyo akifanya yake katika Baadhi ya Mashambulizi.
        

No comments:

Post a Comment

Pages