Tarehe Ya
Kuzaliwa.
Donnie kila ifikapo July 27 ndiyo siku ambayo husheherekea
siku yake ya kuzaliwa ambapo mwaka 1963 ndiyo mwaka aliovuta pumzi ya duniani.
Jamaa kwa ufupi ni Mwigizaji,Mwanamapigano (Martial
Artist),Direkta,Produza wa filamu,Msanifu wa mapigano (Action Choreographer) na
pia mshindi mara kadhaa katika mapigano ya Wushu.
Utoto Wake.
Alizaliwa Guangzhou,China ambapo Mama yake anaefahamika kwa
jina la Bow-Sim Mark ni mwana Mapigano (Martial Artist) wakati Baba yake ni
Mhariri wa gazeti.
Akiwa na miaka miwili,Familia yake ilihamia Hong Kong na
baadae wakahamia Boston,Marekani hapo akiwa na miaka 11.
Akiwa mdogo,Donnie alipenda sana kujifunza mapigano hasa
kutokana na kupendezwa na Mama yake ambae alikuwa akimuona mara kadhaa akifanya
mazoezi.
Alianza kujifunza Tai Chi na Kung Fu, akiwa na miaka 9 tu
lakini alipofikisha miaka 14 alipoacha shule aliamua kuwa serious zaidi ambapo
muda wake mwingi alikuwa akiutumia katika kujifunza Wushu.
Kutokana na hali hiyo,Wazazi wake waliamua kumpeleka Beijing
ili akajifue zaidi katika Wushu na alipomaliza kabla ya kurejea Marekani
alienda Hong Kong ambapo alikutana na Action Choreographer maarufu Yuen
Woo-Ping ambapo Donnie alianza kujifua na Taekwondo akiwa na miaka 16 hapo.
Ukiachana na hayo,Familia ya Donnie unaambiwa pia ni Familia
ya vipaji vya Muziki ambapo Mama yake anaweza kupiga vyema sana Soprano na Baba
yake anaweza kupiga vyema Violin kitu ambacho hata Donnie akiwa mdogo
alifundishwa kupiga Piano akiwa mdogo lakini na Pia anajua vyema sana kucheza
Break Dancing na pia hata Kucheza muziki wa Hip Hop.
Kutambulika
Rasmi alianza kutambulika mwaka 84 baada ya kucheza katika
filamu ya Drunken Tai Chi…mwaka 88 alitokea katika Tiger Cage na baadae pia
katika Once Upon A Time in China sehemu ya 2 iliyoachiwa mwka 92 ambapo
walipambana vyema na mtaalamu Jet Li.
Mwaka 93 alicheza pia katika Iron Monkey pia mwaka 2002
alitokea katika filamu kali pamoja tena na mkali Jet Li.
Tukirudi nyuma utaachaje kuitaja Series kali ya Fist of Fury
ambayo ilikuwa ikioneshwa na chaneli ya ATV ambao walifanya kuhamisha kutokea
filamu yenye jina hilo hilo ambapo ilikuwa imechezwa na mkali Bruce Lee
akitumia jina la Chen Zhen.
SOMA PIA>>MBUZI AKAMATWA KWA KUIBA GARI NIGERIA
Baada ya Series hiyo hapo ndipo Donnie alianza kutajwa kama
ndiye mrithi sahihi wa Bruce Lee hasa kutokana na kazi nzito aliyoifanya.
Mwaka 2010 kitu kilirudiwa kwa utofauti ikipewa jina la Legend
of the Fist:Return of Chengzhen ambapo moto uliwashwa zaidi.
PITA HAPA PIA>>WAKALI WOTE WA KICHINA NDANI YA FILAMU MOJA
Alianzisha kampuni yake ya Filamu aliyoipa jina la Ballistic
Films ambayo iliweza kuandaa filamu kadhaa kama Legend of the wolf na Ballistic
Kiss ambazo ndani pia alicheza yeye.
Kuanguka kimtindo na Kuamka
Tena.
Katika maisha kuna changamoto,Nae pia alipitia changamoto
ambapo katika kampuni yake kazi kadhaa walizoandaa hazikufanya vizuri sokoni
hali iliyopelekea Donnie kufilisika ambapo ili mlazimu kukopa pesa ili
kuinusuru kampuni yake.
Baada ya kazi nzito akiwa Hong Kong,Aliamua kwenda Marekani
ambako alifanya kazi katika filamu mbili kama Action Choreographer…filamu ya
Highlander:Endgame na Blade 2 kazi iliyompa sifa kadhaa na baadae kuzidi kumpa
michongo mingine kama Hero.
Alifanya kazi nyingi ambazo ziliweza kufanya vizuri kama
SPL,Shaghai Knigts,Flash Point,Ip Man ambazo pia zilizidi kumpa umaarufu.
Unaambiwa mwaka 2011 pengine tungemuona katika The Expendables
2 lakini Donnie alikataa kushiriki katika Filamu kutokana na kuwa na kazi
zingine.
Kwa miaka ya hivi karibuni kapata sifa kubwa zaidi baada ya
kutokea katika michongo miwili kutoka Hollywood ambayo ni Rogue One:A Star Wars
Story(2016) pamoja na Xxx:Return Of Xander Cage(2017).
Sifa za Upekee.
Donnie anasifika sana kwa kuweza kuipa umaarufu staili ya
mapigano ya Wing Chun ambayo ameitumia katika Filamu za Ip Man,Ambazo ni filamu
zikimuangazia masta aliyefahamika pia kwa jina hilo la Ip Man,ambaye anasifika
kwa kuwa mojawapo ya waanzilishi wa staili hiyo pamoja na kuwa ndiye mtu
aliyemfundisha Bruce Lee.
Baada ya filamu hiyo,Unaambiwa idadi ya watu walianza
kumiminika kutaka kujifunza Wing Chun ambapo hata mtoto wa Ip Man, anamshukuru
sana Donnie kwa kuweza kuipa umaarufu staili hiyo na pia kuweza kusababisha
Baba yake kuendelea kukumbukwa.
Unaambiwa kabla hajaenda kufanya filamu hiyo,ilibidi kuingia
darasani kujifunza ambapo ndani ya miezi 9 aliweza kui masta yoote ambapo kwa
kawaida mtu anaejifunza staili hiyo huwachukua wengi mpaka miaka 3 kuweza
kuimasta vyema kabisa.
Ukiachana na hilo pia Donnie anasifika kwa kuleta staili mpya
ambayo ameipa jina la la MMA yaani Mixed Martial Arts ambapo huwa anamix
mapigano mbalimbali kama umetazama Flash Point,Spl ni mojawapo ya filamu ambazo
alitumia staili hiyo.
MMA ni mjumuisho wa staili mbalimbali kama Tai
Chi,Boxing,KickBoxing,Jeet Kune Do,Hapkido,Wing
Chun,Wushu,Taekwondo,Judo,Wrestling,Brazilian,Karate,Muay Thai na Jiu-Jitsu.
Upande wa Ngumi vipi?
Hapa kama umesoma vizuri tangu juu basi utakuwa ushajua jamaa
ana uwezo gani..kwa kifupi asilimia kubwa ya staili zote za ngumi anazijua na
pia anamiliki hata baadhi ya mikanda katika ngumi katika Taekwondo anamiliki
mkanda mweusi pia Judo na upande wa Wushu anamiliki mkanda wa dhahabu.
Donnie ni mpenzi mkubwa wa UFC mojawapo ya mapambano ya hatari
ambayo wapiganaji hutumia ngumi na miguu ambapo anasema kuwa,Kama asingekuwa
anamatatizo ya kiwiko chake cha mkono alitamani ashiriki siku moja.
PITA HAPA PIA>> SHABIKI KAAMUA KUFANYA UPASUAJI MARA 50 KUFANANA KAMA ANGELINA JOLIE, MATOKEO YAKE AWA KIBWENGO
Watu kama Jet Li,Jackie Chan,Michelle Yeow,Cung Lee wanampa
sifa sana Donnie kuwa ana spidi kali sana katika mapigano na pia yupo vizuri
katika mapigano ya nguvu yani ukiachana na kujua staili nyingi,Ngumi zake huwa
zina nguvu sana.
Mfano katika Ip Man 3, Waandaaji wa Filamu walikuwa na
wasiwasi kwamba Tyson angeweza kusahau miondoko na kurusha ngumi za ukweli
lakini ni Donnie ndiye aliyemuumiza Tyson wakati akipangua ngumi zake.
Hiyo ndo stori kwa uchache ya mtu mzima Donnie Yen, Naimani kuna mambo utakuwa Umejifunza katika Stori nzima...Unaweza ukatuachia maoni yako hapo Chini na pia Usisahau Kutu Follow katika mitandao mbalimbali ya Kijamii @teknomovies
No comments:
Post a Comment