THE FATE OF THE FURIOUS, REVIEW - teknomovies
THE FATE OF THE FURIOUS, REVIEW

THE FATE OF THE FURIOUS, REVIEW

Share This
Hii movie kwanza kama kawaida, imeanza vizuri sana sana Naweza nikasema kwa mafanikio mpaka sasa iliyofikia Kiukweli ina deserve.
Kila actor / actress kafanya kazi yake vizuri pamoja na team nzima ya Waandaaji nao pia wamefanya kazi yao safi.
Ukisema U compare kwa ubora Toka ya 1 mpaka 8 ipi iliyotisha zaidi, jibu moja kwa moja ni kazi kupata sababu kila moja ina ubora wake, ila kimafanikio mpaka sasa iliyotisha zaidi ni Fast n Furious7.
Kuna vingi binafsi nilivyopenda katika huu mzigo, Licha ya uwepo wa magari makali na pia action nzuri... Lakini kuna comedy nzuri unaipata pia... Na safari hii haikua Tyrese pekee anaekupa Comedy bali hata Jason Statham na Dwayne Johnson.
Unajua jamaa walipaniana sana sana, sasa wakawa wanatishiana kwamba Yani wewe siku nikikushika lazima nikufumue Makalio Dwayne huyo a.k.a The rock anamwambia Jason... Afu Jason anajibu hivi Umfumue nani, unafikiri huo mwili unanitisha.... Kwanza walianzia ugomvi wao, wakiwa Gerezani kwa kutukanana.. Nilicheka zaidi walipoanza kubishana eti nani aliyempa kichapo mwenzake kwa mara ya kwanza walipokutana... Sasa The Rock anamwambia yani Wewe Mshenzi Huna lolote na Una bahati yako Ulikimbilia kurusha bomu bila hivyo ningekukamua.. Jason anajibu Umkamue nani?? Mtu gani ulianza kukimbia, ukaamua kuruka kutoka dirishani kama mtoto mdogo.
Walitishiana Wee mpaka kuna sehemu wakaanza kucheka wenyewe..
Sasa hayo mabishano yao, lazima ucheke yani 
Kuna scene niliipenda wakati kimenuka gerezani kuna jamaa lilikua na Beef na The rock, sasa likawa linamfuata Ili kwenda kumuattack huku likiongea Yani hii moment Niliisubiri kwa Muda sanaaa.
Lilipigwa Kiki mbili Tu... Afu akajibu Keep Waiting Bitch...
Nimependa kazi ya Vin Diesel, kafanya kazi yake ipasavyo.. Naweza nikasema Jamaa ni Bonge sana La Actor.. Jason ndo kaua zaidi... Mama wa Ngwasuma Charlize Theron nae zaidi.
Kuhusu Story line ni Ya kawaida Tu kama zingine sio ya kuumiza sana kichwa... Unaweza ukawa unafanya chochote ama unachati na ukaelewa.. Cha msingi kwako mpenda movie hii sio movie ya kukosa kutazama kwako...
Kitu kingine Uwongo nao umezidi sana, na umezidi kukua zaidi ukitofautisha na zingine zilizowahi kutoka.. Ila Uongo wao ni ule wa kukuaminisha na kweli utaamini, ila tunaojua wanavyofanya ndo tunajua uwongo wao.. Ebu Tusubiri FAST 9 inayotegemewa kutoka mwaka 2019 Tuzidi kuomba Uzima.

No comments:

Post a Comment

Pages