Mohra (Kamba) ni filamu ya kihindi
Yenye mahdhui ya kisiasa iliyoongozwa na director Rajiv Rai(huyu director ndo ali direct pia movie ya vishwatma na Gupt) huku mstaa wakiwa ni Akshay Kumar, Sunil Shetty, Raveena Tandon na
Naseeruddin Shah na wengine ni Paresh Rawal, Gulshan Grover,
Raza Murad na Sadashiv Amrapurkar ambao walikuwa kwenye kusaidia majukumu.
filamu ilitoka tarehe 1 Julai 1994 na ilikuwa ya pili kwa mauzo ya filamu za kihindi mwaka 1994. Bajeti ya movie ilikuwa ni $ 560,000 na mauzo yalikuwa $ mil 3.4.
Pia Filamu hii ilipata kuteuliwa mara tisa katika tuzo za filmfare mwaka 1995. Ilikuwa ni mara ya kwanza Akshay Kumar, Sunil Shetty na Paresh Rawal kufanya kazi kwa pamoja.
Awali Divya Bharti ndie alipangwa kuchukuliwa kwa kuongoza scene ya mwanamke lakini baada ya kufariki mwanadada Raveena Tandon akachukua nafasi hiyo badala yake.
Filamu hii pia inakumbukwa kwa nyimbo zake ambazo nyingi ziliingia kwenye chart ya Chartbusters katika mwaka huo.umaarufu wa wimbo "Tu Cheez Badi Hai Mast Mast", ambayo ilikuwa inaimbwa kwa ustadi mzuri na Raveena Tandon ikasababisha dada huyo kupewa jina la utani “Mast mast Girl”.
No comments:
Post a Comment