Ni kawaida ukiingia kwenye usafiri aidha wa gari ama wa ndege kukuta mikanda kwenye viti vya abiria lakini hali hii ya kuwepo kwa mikanda hujawahi kuishuhudia kwenye treni. Ukweli ni kwamba hakuna mikanda kwenye viti vya abiria kwenye treni zote duniani.
Zipo sababu kadhaa za kutokuwepo kwa mikanda kwenye viti vya treni .
Kwanza treni za kasi zinakwenda bila kutetemeka. Abiria mmoja aliwahi kufanya majaribio ya kusimamisha sigara kwenye meza ya treni ambayo ilikuwa ikienda kwa kasi ya kilometa 300 kwa saa na sigara hiyo haikuanguka.
SOMA PIA: DJ KHALED AWA BALOZI WA KUPUNGUZA WATU UNENE
Lakini pia mikanda kwenye treni inawadhuru abiria badala ya kuwaokoa . Kamati ya usalama na vigezo vya reli ya Ulaya iliwahi kufanya uchunguzi na kugundua kuwa wakati ajali inapotokea ni rahisi zaidi kwa wanaofunga mkanda kwenye viti kujeruhiwa kwani hawawezi kutoka.
Na sababu nyingine ni kwamba abiria hawapendi kufungwa kwenye viti vya treni, wanapenda kutembea zaidi kwenye mabehewa.
Lakini kwa nini tunatumia miknda kwenye ndege na gari? . Ndege inapokumbwa na upepo hutetemeka angani kama abiria hawatumii mikanda kwenye viti wananweza kujiginga na paa,viti au sakafu na magari yanaposimama au kugonggana ghafla watu watajigonga na usukani, vioo na viti au hata kutolewa nje ya gari. Hivyo ni muhimu kufunga mikanda kwenye ndege au gari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment