MAPENZI YAO YALIANZIA LOCATION, SASA NI WANANDOA. - teknomovies
MAPENZI YAO YALIANZIA LOCATION, SASA NI WANANDOA.

MAPENZI YAO YALIANZIA LOCATION, SASA NI WANANDOA.

Share This
Waswahili wanasema “Penzi ni kikohozi kulificha huwezi” hii imetokea kwa baadhi ya wasanii duniani ambao mapenzi yao yameanzia wakiwa
Location wakishoot movie na sasa ni wanandoa na wana watoto. Hii ni list ya wasanii kutoka Bollywood.

Abhishek Bachchan & Aishwarya Rai Bachchan

                             

Kwa mara ya kwanza walikutana wakiwa wanashoot movie ya  Dhaai Akshar Prem Ke na Kuch Naa Kaho, wakawa kama marafiki. Lakini kumbe kiuhalisia kila mmoja alikuwa kamzimikia mwenzake ingawa walioneana aibu kwa wakati huo. Mwaka 2006 walipokutana tena location kwenye kutayarisha movie 3 kwa mpigo  Umrao Jaan, Guru na Dhoom 2 hapo wakatumia muda mrefu kuwa pamoja na taratibu kila mmoja akamsoma mwenzake kihisia na Mwisho wa siku mwaka 2007 wakafunga ndoa rasmi.


Saif Ali Khan & Kareena Kapoor Khan

Mwaka 2007 baada ya mahusiano ya Kareena Kapoor na Shahid Kapoor kuvunjika ndipo mwaka huo huo Bebo (Kareena Kapoor) akaanza kushoot filamu ya Tashan na Bollywood Star Mr Saif Ali Khan. Mapenzi yalikuwa moto hasa walipokuwa location nzuri za Kerala, Ladarkh, Rajasthan na Hridwar. Walikuwa wapenzi takriban miaka 5 na mwaka 2012 wakajisajili kama wanandoa (Wakafunga Ndoa).

saif na mke wake kareena kapoor

 Ajay Devgn &Kajol

Huenda watu wengi wakaamini Kajol na Shah Rukh Khan ni wapenzi hii ni kwa sababu ya scene kali za kimahaba kwenye filamu ya Kuch Kuch Hota hai lakini ukweli ni kwamba Kajol ni mke halali wa Ajay Devgn. Walikutana kwenye movie ya Hulchul mwaka 1995 na waka date kwa miaka 4 na ilipofikia mwaka 1999 wakafunga ndoa rasmi. Kwa sasa wana watoto wawili Nysa na Yug na hivi karibuni walisherehekea miaka 18 ya ndoa yao.

ajay na kajol katika pozi pamoja

 Akshay Kumar &Twinkle Khanna

Walikutana kwenye scene za movie mbili Khiladi na Zulmi. Mapenzi yakawa mubashara na mwaka 2001 wakaingia ndoani, kwa sasa wana watoto wawili wa kiume.

Akhshay na mke wake

 Amitabh & Jaya Bachchan

Story ya mapenzi kutoka kwa hawa masupastaa wawili wa Bollywood ilianzia wakiwa location wakishoot movie ya Zanjeer. Kipindi hicho Jaya Tayari ni Superstar na Amitabh yeye ndo alikuwa anapambana ili afahamike (Underground Actor). Kilichopelekea kuwa wapenzi watu hawa na hadi kuoana huenda kikafurahisha sana , Amitabh ali share story na watazamaji wa show ambayo anaiendesha inayoitwa Kaun Banega Crorepati. Wawili hawa walipanga kwenda London endapo movie yao ya Zanjeer ikipokewa vizuri na mashabiki. Kweli movie ikapata mafanikio kinoma kwenye Box office na ndipo wakapanga safari ya kwenda London

Baba yake Mkubwa mkubwa Amitabh Mr Harivansh Rai Bachchan  aligomea safari hii kwa mtoto wake kwa sababu alijua tu nini kitatokea huko ukizingatia bado hawajaoana, ndipo wakaambiwa kama wanataka kwenda London lazima waoane, Unaambiwa siku hiyo hiyo mama akakubali aolewe.


Basi harusi ikapangwa wakafunga ndoa na wakaenda London na hadi leo ni mke na mume na Tareh 3 June watasheherehea miaka 44 ya ndoa yao.

Amitah akiwa na mke wake katika pozi zuri.

 

Pages