Rosa Ree : Nilianza Kuimba Kabla Ya Kurap - teknomovies
Rosa Ree : Nilianza Kuimba Kabla Ya Kurap

Rosa Ree : Nilianza Kuimba Kabla Ya Kurap

Share This
One time ndio ngoma ambayo ilimtambulisha vyema sana katika gemu la Bongo Fleva huku sauti yake pamoja na mashairi yake kwa watu wengi ilionekana ikiwa katika utofauti mkubwa sana huku akitokea katika lebo kubwa Bongo ya The Industry  ikiongozwa na wakali kama Navy Kenzo ambao ndio wamiliki wa lebo hiyo,Wildad pamoja na jina hili ambalo leo unalisoma muda huu,Rosa Ree.
Mpaka sasa ameweza kuachia ngoma tatu ambazo zinazidi kukimbiza katika vituo mbalimbali vya habari ambazo ni One Time,One Time remix ambayo alifanya na rapa kutoka Kenya,Khaligraph Jones,Up In The Air pamoja na kazi ya Mchaga Mchaga ambayo amefanya na mabosi zake Navy Kenzo.

Dili na The Industry?

“Muziki nilianza tangu muda sana tangu nikiwa shule na tena nilikuwa naimba kipindi hicho na kuna ngoma kadhaa nilitoa ambazo nilikuwa naimba lakini hazikufanya poa,”

“Nilianza kuchana pia nikakuta watu wanapenda sana nikichana so nakumbuka ilikuwa mwaka 2015 nilienda kwa Nahreel kurekodi ngoma alivyonisikia tu alipenda sana,”


“Hivyo baadae aliniomba niwe kwenye lebo yake nilifurahi kwanza alafu sikuamini lakini ndio ikawa hivyo nikasaini hapo,mpaka sasa napiga mzigo,”

Mishe zingine vipi?

“Mimi nafanya Biashara pia lakini mambo yangu mimi napenda kuyaweka kwa siri sana hivyo siwezi kusema ni biashara gani mpaka mambo yangu fulani yatimie nahisi naweza sio nitasema,ila nahisi naweza kusema.”Aliongeza.

Nini Kinafuata baada ya mchaga mchaga?

“Baada ya Mchaga Mchaga kuna ngoma kali sana inakuja yani hapa nasubiri tu wakati uwadie kitu tukiachie na pia nafikiria kutowachosha mashabiki zangu sababu nataka kuachia ngoma kali kwa kila kipindi Fulani.” Alisema.


“Na pia kuhusu video ya Mchaga Mchaga mipango bado ipo inafanyika ili kuja na kitu tofauti kama unavyojua Rosa Ree tangu nitoke kwenye upande wa video nikiri sijawahi kuzingua na hivyo najipanga kuja na jiwe kali sana.” Aliongeza.

Kolabo na Rapa wa Kenya?

“Aisee hii kolabo nikiri imenipa mafanikio makubwa sana,kwanza imeniongezea sana mashabiki kwa upande wa Afrika Mashariki kwa ujumla na mafanikio mengine ambayo siwezi kuyaweka wazi ila kiukweli nimepata mafanikio niliyotarajia,” Amesema.

Staili yake vipi?

Moja ya jambo kubwa ambalo mara kadhaa amekuwa akikumbana nalo ni watu kadhaa wamekuwa wakimkosoa hasa staili yake ya mavazi ambayo watu wanadai yapo nje ya maadili ya Kitanzania pamoja na matumizi ya maneno katika nyimbo zake ambayo  yamejaa matusi sana.
“Mimi sifikirii hata kidogo kubadirika sababu eti kwa maneno ya watu sababu kuwa orijino ndicho kitu cha msingi alafu ukifuata kila kitu watu wanasema ni kazi sana kufanikiwa chamsingi mi sitobadirika bali nitazidi kuwa bora zaidi sababu naamini kuna watu wanapenda ninachokifanya,”

Watu wasichojua kutoka kwake?

“Kuna vingi wengi hawajui kutoka kwangu,huwa wanaweka vitu vyao kutokana na namna wanavyoniona,Lakini kiukweli mimi napenda sana sana watoto alafu pia situmii kilevi chochote kuna watu huwa hawaamini lakini ukweli ndio huo,”

Kama sio Muziki basi angekuwa anafanya nini?

“Ningekuwa Daktari aisee kama sio Muziki maana ni kitu ambacho tangu muda kilikuwa akilini mwangu kwahiyo kama nisingekuwa nafanya Muziki basi sahizi ningekuwa nacharika na wagonjwa Hospitalini,”
Vitu ambavyo hapendi.

“Mimi sipendi watu wanaochonga chonga,watu wambea mbea na pia watu wakiongea vitu vibaya kwa mwingine pia sipendi mtu mnafiki mtu ambaye anafanya vitu ili kumshusha mtu fulani yani sipendi sana asikwambie mtu,”

Shoo ambayo hatokuja kusahau.

“Sitokuja kusahau shoo ya “Castle Light Unlock” kiukweli shoo nyingi huwa napata shangwe sana ila hiyo shoo nakumbuka nilipafomu wimbo wa Mchaga Mchaga ambao ulikuwa bado haujatoka na watu walikuwa wakiitikia ilinipa sana nguvu asikwambie mtu,”

Vitu ambavyo hapendi kuja kuvifanya kabisa.

“Kitu ambacho sifikiri kabisa kuja kufanya ni Siasa,mimi sipendi kabisa siasa na sifikiri kabisa sijui kwa mbele itakuaje ila mimi akili yangu inaniambia hivyo kwamba Rosa Ree siasa wewe kwako haipo,”

Albamu na Mixtapes(Kanda Mseto) vipi?

“Mipango ipo sema nafikiri bado mashabiki zangu wanahitaji singo zaidi ili kuwatengenezea nafasi zaidi ya kuja kufurahia albamu yangu ila mipango ipo na pindi itapowadia watu wataona,”

 Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.





Pages