YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-7 - teknomovies
YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-7

YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-7

Share This
Ilipoishia……..

Wakati wanatoka katika ukumbi wa MGM Grand, Tupac aliona mtu akipora cheni kwa mmoja wa watu waliokuwepo kwenye mechi hiyo, jamaa aliyeporwa hakukubali wakaanza kuzichapa na hapo Tupac aliamua kuingilia ugomvi huo, kumbe ugomvi ulikuwa ukihusisha vikundi viwili kutoka West Coast Side vikundi hivyo vilijulikana kwa majina ya Crips na Bloods. Wakati hayo yote yanatokea Suge alikuwa akishuhudia kwani aliamua kufuatilia kila tukio analofanya tupac usiku huo .


Endelea…..

Kabla ya kuendelea ni vema tuyajue haya makundi mawili ya Crips and Bloods. Haya ni makundi ambayo asili yake ni West Coast Side, umaarufu wa makundi haya ulitokana na utukutu wao, ni vikundi ambavyo vilikuwa vikiishi kwa kulipiza visasi ambapo kauli mbiu (Slogan) yao ilikuwa ni “Eye for an Eye”. Kwa maana hiyo matukio yoyote ambayo hutokea katika mji huo basi huonekana hawa ndio wamefanya kwani tabia yao inajulikana.
Baada ya kumalizika kwa vurugu za kugombea cheni, Tupac akarejea Hotelini kwa ajili kujiandaa na show katika club ya 662. Akiwa hotelini girlfriend wake alimuomba ajumuike nae kwenye show hiyo lakini alimkatalia, mpaka leo hakuna anaejua kwa nini alimkatalia, achana na hilo pia Tupac huwa anavaa Bullet Proof (vazi la kuzuia risasi) lakini siku hiyo hakuvaa na hakuna anaejua kwa nini siku hiyo hakuvaa.

Tupac aliingia kwenye gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na Suge Knight na gari ya Bodyguard ilikuwa nyuma ikiwafuata, walipofika njia panda ya Kovak Lane wakasimama kusubiri waruhusiwe na taa. Wakati wanasubiri kuruhusiwa pembeni yao ilikuwa inakuja gari aina ya Cadillac yenye rangi nyeupe ikiwa kwenye mwendo wa taratibu ikasogea hadi iliposimama gari ya Suge (ambapo ndani yake amepanda Tupac). 

Tupac alikuwa ameketi kwenye kiti cha abiria, mara ghafla ikachomolewa Bastola kutoka kwenye kioo cha gari ile aina ya Cadillac na wakamuelekezea Tupac, hawakuwa na muda wa kusubiri walizifyatua risasi kadhaa na zote zikampata Tupac . Baada ya tukio hilo ile gari ikaondoka kwa speed kali na hapo Bodyguard wa Tupac akachomoka kwenye gari na kumkimbilia Tupac ili amsaidie.

Baada ya tukio, gari la Suge Knight lilikaa pale pale kwa muda mrefu na katika utetezi wake alisema alichanganyikiwa na tukio lile hivyo hakujua la kufanya. Hapa nadharia ya kuwa alihusika inazidi kushika kasi kwani inaaminika lengo la kubakisha gari hapo bila kufanya lolote litamhakikishia Tupac kutopata msaada wa haraka hivyo kupoteza maisha. Kitu kingine ni kwamba katika moja ya Interview Suge alisema hata yeye kuna risasi ilimpata ya kichwa lakini ulipofanyika uchunguzi ikagundulika hakuna risasi iliyompata zote zililengwa kwa Tupac.

Mbali na hilo Suge pia alisema baada ya tukio kutendeka walitumia dakika chache kuzungumza na Tupac akiwa na majeraha huku akionyesha tabasamu lakini uchunguzi wa madaktari ulionyesha kuwa baada Tupac kushambuliwa kwa risasi alipoteza fahamu pale pale, swali likawa Suge alicheka na nani? Hizo ndizo sababu kuu zinazoashiria Tupac aliuawa na Suge, vipi wewe mtazamo uko kwa nani? Acha Comment yako.


Itaendelea………….

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.


Pages