Kwanini Hautakiwi Kukosa Kutazama Filamu Hii #Uchambuzi - teknomovies
Kwanini Hautakiwi Kukosa Kutazama Filamu Hii #Uchambuzi

Kwanini Hautakiwi Kukosa Kutazama Filamu Hii #Uchambuzi

Share This

Watu wanapenda Filamu lakini kila mmoja anaweza akawa na aina za filamu anazopenda kutazama mara nyingi zaidi.

Mfano mimi napenda sana kutazama Filamu za Action japo huwa natizama filamu nyingine lakini katika Kompyuta yangu utazipata filamu nyingi zimejaa za Action.

August 18 mwaka huu Filamu ya The Hitman's Bodyguard iliachiwa ambapo iliwakutanisha wakali wawili Ryan Reynolds anaefahamika vyema kwa kukinukisha katika Filamu ya Deadpool pamoja na mtaalamu wa Kitambo Samuel L Jackson.

Kuna mambo kadhaa ambayo nataka nikuambie juu ya hii Filamu na kwanini Uitafute kama bado.

Story Line: Ni filamu ambayo story yake imekaa Simple sana, mtu yeyote ni rahisi kuielewa ikiwa inamzungumzia Bodyguard ambae ni Ryan akiwa anatakiwa kumlinda muuaji hatari ambae ni Samuel kwaajili ya kwenda kutoa ushahidi kutoka England mpaka mahakamani The Hague ambapo kabla ya kazi hiyo nyuma wote wawili walikua wakitafutana sana ambapo Ryan anamtuhumu Samuel kua ndiye alimuharibia kibarua chake kwa kuweza kumuulia baadhi ya watu aliopewa dili kwaajili ya kuwalinda.

Wakiwa njiani kuna mengi yanatokea ambapo Samuel anawindwa vikali ili kuwawa asiende kutoa huo ushahidi na kuifanya Filamu kupendeza zaidi na zaidi hivyo story haiumizi kichwa hata kidogo.

 Vichekesho: Moja ya jambo waliloweza kufaulu vyema ni suala la vichekesho ambapo kama ushawahi tazama filamu zao za nyuma wote wawili basi unajua uwezo wao mzuri katika kuchekesha.
katika Filamu wameweza kutisha sana katika vichekesho na huku ukiendelea kuburudika na ngumi za hatari.
Chemistry: Kitu kizuri zaidi ndani utachofurahi ni uwepo wa muungano mzuri sana wa Ryan na Samuel. Filamu hii imeweza kuweka muungano wao mzuri kiasi kwamba utapokua unatazama muda wote unatamani uwaone wao Tu. Kitu poa hapa ni kua uhusika wao ulikua bora na kama umewahi kutazama Bad Boy ya kwake Will Smith na Martin Lawrence na ukaipenda basi hii inaweza kukufaa zaidi.

Haina Mzunguko: Katika filamu hii kitu kizuri zaidi ni kila kitu kipo katika Mtiririko wa Barabara kwamba hakuna sijui vikwazo vitavyokufanya kuanza kutaka kurejea nyuma kwa maana kwamba utapoanza kutazama mpaka utapomaliza filamu imepangwa katika mstari mnyoofu.

Unapenda Black American Movies? basi hapa pia ni mahala pako. Kwa wapenzi wa filamu hizo huwa wanajua jinsi namna Ma black wanavyoongea na mambo mengine.
katika hii filamu Samuel kaweza kuinogesha vizuri na maongezi yao ya Matusi ya kutosha pamoja na Ryan unaweza Jisahau kama nae Ryan ni Mzungu.
Hayo ni kwa upande wangu kama nawe umetazama,weka hapo Chini Comment yako Kuongeza mengine uliyoyapenda zaidi.

Usisahau kutucheki Instagram na Twitter @Teknomovies Kwa habari mbalimbali.

Kwa mahitaji ya Filamu hii na pia zingine unaweza kuwasiliana kwa kutumia Mtandao wa Whatsapp kupitia Namba hii 0625716354.

Bonyeza Play Hapo chini kutazama Trailer Yake.

             

Pages