Nchi nyingi za kiarabu zimekuwa na sheria nyingi ambazo zimekuwa kwa namna moja ama nyingine zikionekana kukandamiza Wananchi, Ukiachana na Sheria ya Wanawake kutokuruhusiwa kuendesha magari bali pia Ishu ya kutokutazama Filamu katika Majumba ya Sinema hasa za magharibi imekuwa ikitekelezwa.
Nchi ya Saudi Arabia, Baada ya mwezi Septemba kuruhusu Wanawake kuendesha magari Sasa imeruhusu pia watu kutazama Filamu katika Majumba ya Sinema.
Ruhusa hiyo imetolewa na Mwana wa Mfalme wa Taifa hilo, Prince Mohammed Bin Salman akishirikiana na Baba yake,King Salman na imeelezwa kuwa itaanza kutekelezwa Mwakani.
SOMA PIA>>CAMILA CABELLO MWANAMUZIKI ASIEJULIKANA
Lakini Filamu hizo itabidi ziwe na maudhui mazuri na zisiwe za kuonesha matendo ya ngono.
Tuachie maoni yako Juu ya hili, Unalionaje kwa upande wako?
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.
No comments:
Post a Comment