The Rock Na Mr Transporter Wameamua Kufanya Laivu Sasa - teknomovies
The Rock Na Mr Transporter Wameamua Kufanya Laivu Sasa

The Rock Na Mr Transporter Wameamua Kufanya Laivu Sasa

Share This
Wakati Fast And Furious sehemu ya 9 ikisogezwa mpaka April 10 mwaka 2020,mjadala unaoendelea kwa sasa katika mitandao mingi ni juu ya ishu ya Dwayne Johnson “The Rock” na Jason Statham kuja na filamu ya pamoja ambayo imetokana na uhusika wao katika Fast and Furious.

Ikumbukwe kuwa jamaa kuanzia Sehemu ya saba walicheza kama maadui ambapo wakosoaji mbalimbali waliwapa sifa kutokana kuleta muunganiko mzuri ambapo katika sehemu ya nane muunganiko wao ndio ulizidi kutisha zaidi na hivyo Universal Studios kuanza mchakato wa kuandaa filamu ya wawili hao.

SOMA PIA:MAKUNDI MAWILI HASIMU YA HIP HOP MAREKANI

Ishu hiyo ilileta mijadala kadhaa huku Tyrese Gibson akitoa mapovu kadhaa kwenda kwa The Rock ambapo ishu kubwa ilikuwa juu ya tetesi hizo huku Tyrese akilalamika kwamba jamaa anahasi kambi jambo ambalo halipendezi kwa sababu wao ni kama timu.

Kwa taarifa yako sasa ni kuwa Chris Morgan ndiye ambae amepewa kazi ya kuandaa Script nzima na kwa taarifa tu ni kuwa filamu hiyo inatazamiwa kuachiwa tarehe 26 July mwaka 2019 nazani mipango yote hiyo itakuwa imefanywa ili kuruhusu kuwepo kwa nafasi ambayo itazipa zote filamu mbili kuweza kuuza vyema sokoni.

Bado filamu hiyo haijafahamika itapewa jina gani,lakini kufikia mwakani jina linaweza kufahamika mapema ili kutoa muda muafaka wa promo zaidi.


Pages