Mbali na
hilo Suge pia alisema baada ya tukio kutendeka walitumia dakika chache
kuzungumza na Tupac akiwa na majeraha huku akionyesha tabasamu lakini uchunguzi
wa madaktari ulionyesha kuwa baada Tupac kushambuliwa kwa risasi alipoteza
fahamu pale pale, swali likawa Suge alitabasamu na nani?.
Endelea……..
Kwa ujumla hiyo ndio hali halisi na hatua zote
alizopitia Tupac mpaka alipoaga dunia, Suge amebeba kikombe cha lawama hii ni
kwa sababu ya tamaa zake alizozionyesha wazi wazi kuhusu fedha ila ndo hivyo
tayari yameshatokea tunabaki kukumbuka tu.
Tupac anabaki kuwa shujaa, amefanya kitu kikubwa
sana kwenye uso wa dunia kamwe hawezi kusahaulika. Amewahamasisha (Inspire)
vijana wengi kwenye muziki na hata nje ya muziki, binafsi pia nimekuwa inspired
na Tupac kutokana na lifestyle ya kuwa halisi (real) pamoja na maneno ambayo
mara nyingi alikuwa akiyatamka na kubaki kwenye kumbukumbu. Mungu ailaze mahali
pema peponi roho yake…Ameeen…!!!!!!
Pamoja na mabaya aliyoyafanya lakini ukweli ni
kwamba likitajwa jina lake basi ni yale mapinduzi yake ndio yanakumbukwa huwezi
kujidanganya nafsi yako kwa kukumbuka maovu yake na kuacha mema aliyoyatenda,
utakuwa unajidanganya. Ni zaidi ya miaka 20 sasa imepita tangu kifo chake
lakini kila mwaka hukumbukwa, ni kwanini hisia zote zinaangukia kwake? Kwa
sababu ya namna alivyoishi.
Utofauti wa Tupac na wasanii wengine ulikuwepo
kwenye mfumo wa utendaji kazi, Tupac alipenda mno kujichanganya pengine hii
ndio ilikuwa sababu ya kuchukiwa na wengi, ilikuwa ngumu kumkuta amejitenga.
Alikuwa anaijua fitna ya muziki vizuri tu.
Kwangu mimi Tupac amenifundisha namna ya kufanya
biashara yako ipate wateja, pamoja ya kwamba mimi si mwanamuziki lakini somo
hili nimelipata kupitia mziki wake. Tupac alikuwa anajua namna ya kuandaa lyrical
(mashairi) yatakayouza kwenye jamii. Inawezekana si wote watakaonunua kazi yake
lakini target yake ilikuwa ni lazima ukisikie kile anachoimba ili hata ukikaa
ufikirie Tupac ameimba nini. Sikiliza wimbo wa Dear Mama na tafakari namna
alivyowajumuisha watu wote kupitia wimbo huo. Sio mabosi na heshima zao, sio
wahuni, sio kinamama bali wote walipenda mashairi yaliyopo ndani.
Mfumo huu wa muziki naufananisha na kijana wetu wa
hapa Bongo Diamond Platnumz, Maisha yake nje ya muziki ni hovyo hovyo lakini
linapokuja suala la kufanya kazi anakuwa serious. Hii ni trick nzuri sana kwa
wanamuziki, Tutakukumbuka Tupac milele na milele.
Maisha ilibidi yaendelee hakukuwa na namna, pamoja
na watu kuhuzunika juu ya kifo chake lakini inabidi maisha yasonge. Ngome zote
mbili (East na West) zilipata baridi kwa muda kwa kumpoteza kijana wao ambae
anaichangamsha game, kijana ambae ukiwa na beef nae hata kama mnachukiana basi
una enjoy.
Ukumbuke ni vichwa viwili tu ambavyo vilitazamwa kwa jicho la
ushindani kwenye game ambao ni Tupac, Biggie Notorious. Biggie akawa amebaki
mwenyewe, ingawa yeye binafsi aliona hiyo ndo time ya kung’aa kwenye ramani
kwani pamoja ya kuwa na beef na Tupac lakini dunia ilikuwa inamuelewa zaidi
Tupac kuliko yeye, wajibu wake uliokuwa mbele ni kuhakikisha na yeye anajenga
umaarufu kama wa Tupac au pengine zaidi.
Itaendelea…….
Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.