YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-5 - teknomovies
YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-5

YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI-5

Share This
Ilipoishia……………

Baada ya kufariki mtu wa kwanza kunyooshewa kidole juu ya mauaji hayo ni Suge Knight , tofauti na inavyodhaniwa kuwa ni Biggie na Puff Daddy ambao hawa walidhaniwa kuhusika kwenye tukio la awali la Tupac kupigwa risasi akiwa studio, Sasa kwa nini Suge Knight amenyooshewa kidole yeye kuhusika na mauaji haya ? .

 Kama hukusoma sehemu ya 4 >>>>>>SOMA HAPA 


Endelea…………

Tupac Shakur kwa mara ya kwanza alisainiwa katika record label Interscope mwaka 1991 na alidumu hapo hadi mwaka 1995. Katika kipindi hicho chote Tupac alikuwa akihusishwa kwenye skendo mbalimbali hasa hasa za beef na wasanii wenzake lakini label hiyo iliamua kumsaini kwa sababu skendo hizo zilikuwa zikimfanya auze zaidi muziki wake sokoni hivyo kwa lugha rahisi unaweza kusema alikuwa na skendo zenye manufaa kwenye biashara.

Pamoja na skendo zote hizo label hiyo ilikuwa ikimlipa kama kawaida lakini mahusiano yake na label hiyo yalivurugika siku ambayo aliingia kwenye kashfa ya unyanyasaji wa kingono na mwanamke mmoja akiwa hotelini hapo mahusiano baina yao yalisamabaratika kutokana mitazamo hasi aliyokuwa akipokea kutoka kwa mashabiki wa mziki pamoja makundi yanayotetea haki za kijinsia.


Swali ni Je urafiki kati ya 2pac na Suge Knight ulianzaje? Ok ngoja nielezee namna urafiki wao ulivyoanza. 2pac alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kutokana na tukio hilo alilolitenda na wakati akiwa huko jamii nzima ilikuwa inamsema kwa mabaya kwani hakufanya jambo la kiungwana kabisa, jamii ilikuwa ikimsema vibaya hakuna mtu aliyekuwa upande wake, kila mmoja alichukizwa na tukio hilo lakini Suge Knight alikuwa tofauti na wote hao, alitumia mwanya huo kumshawishi Tupac akitoka gerezani ajiunge kwenye record label ya Death Row ambayo aliianzisha yeye na Dr Dre  na kwa hali hiyo alifanikiwa kumshawishi 2Pac kujiunga na label hiyo.

Kutokana na Tupac kukaa nyuma ya nondo kwa muda, huku mtaani mfumo wake wa biashara ya muziki ulivurugika na ilihitajika nguvu kubwa kuujenga tena msingi wake, Suge akatumia chance hiyo kwani kivyovyote vile Tupac alitaka kurudi kwenye game hivyo angekubaliana na lolote lile atakaloambiwa na Suge. 



Finally Tupac akasainiwa kwenye record label ya Death Row, jukumu lake kubwa likawa ni kubadilisha image ambayo ilikuwepo kutokana na tabia zake. Jukumu lake kubwa likawa ni kutengeneza ngoma tu na si kingine. Kutokana na hasira alizokuwa nazo jamaa akawa anarekodi nyimbo tatu kwa siku yani anaamka studio na analala studio na hapo akakamilisha album ya “All Eyez On Me” ambayo imekuwa album bora kabisa.

Kutokana na album ya Tupac kufanya vizuri sokoni, Death Row Record ikawa maarufu, Tupac akawa kama balozi wa kuitangaza record label hiyo kila pembe ya Dunia na hapo Suge na Tupac wakawa washkaji kiasi cha kwenda ‘Out’ pamoja. 

Tupac alidhamiria kabisa kujibadilisha kabisa kutoka tupac aliyezoeleka kama mtata hadi kuwa Tupac ambae aonekane ni nguzo kwenye jamii.  Akaanza kuwa karibu na jamii zaidi kwa kuandaa event mbalimbali hasa katika vituo vya watoto yatima akawa anatoa misaada tofauti mpaka kufikia hatua ya kutaka kuingia kwenye siasa.



Matukio haya yote yalikuwa yakiratibiwa na record label yake chini ya C.E.O Suge Knight ingawa Suge hakupenda label yake ishiriki kwenye mambo haya kwani walikuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye misaada lakini alishindwa kumwambia Tupac juu ya suala hilo kwani yeye ndo anaeleta faida kubwa kwenye label yake sasa akimwambia si atavuruga biashara? Ikabidi avumilie tu na ashiriki kishingo upande. Kikubwa kilichomuumiza ni siku waliyotumia takribani $ 60 million kwa ajili ya msaada, hili Suge lilimuuma mno.


Itaendelea…… 


Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube channel ya DM Online Tv.


Pages