NANDY AMKIMBIZA DIAMOND PLATNUMZ YOUTUBE - teknomovies
NANDY AMKIMBIZA DIAMOND PLATNUMZ YOUTUBE

NANDY AMKIMBIZA DIAMOND PLATNUMZ YOUTUBE

Share This
Kwa mwaka 2017 ni hakika Nandy hawezi kuusahau kwani ndio mwaka ambao safari yake ya mafanikio ilikuwa juu zaidi..Ukiachana na Tuzo ya Afrimma lakini pamoja na kufahamika sana kwa dau wengi.
Kwa sasa Nandy anakimbiza na ngoma ya Kivuruge ambayo Desemba 19 aliachia video yake rasmi katika mtandao wa Youtube.

Mpaka sasa ndiyo video inayoshikilia namba moja kama video zinazokimbiza zaidi katika mtandao wa Youtube huku ikiwa imeiacha video ya Diamond Sikomi ikiwa inakamata nafasi ya 24 ambayo kwa wiki kadhaa ilikamata nafasi ya kwanza.

SOMA PIA: TECNO SPARKS TOLEO LIPYA NAFUU KWA WATU WENGI

Kwa video zinazofuata zionazokamata namba 2 na kuendelea ni Video za kawaida ambazo sio za wasanii ambapo mpaka namba 23 ambapo imekamatwa na Video ya Young Killer Ft Bright - Toto Tundu Kisha inafuata video ya Diamond.

Mpaka Sasa Video ya Nandy imekusanya watazamaji zaidi ya Laki tano ambapo yupo kuitafuta Milioni Moja, vipi unafikiri ataifikia hiyo?

Pamoja na hivyo kukimbiza Youtube,muda wowote List inaweza kubadilika kutokana na video kila siku kuendelea kuachiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages