Huyu Ndio Binadamu Mchafu Zaidi,Hajaoga Zaidi Ya Miaka 60,Na Yupo Anasaka Mke - teknomovies
Huyu Ndio Binadamu Mchafu Zaidi,Hajaoga Zaidi Ya Miaka 60,Na Yupo Anasaka Mke

Huyu Ndio Binadamu Mchafu Zaidi,Hajaoga Zaidi Ya Miaka 60,Na Yupo Anasaka Mke

Share This
Huyu mzee hana mke lakini anatafuta Mke, Ambapo ili uwe Mke wake basi inakubidi ukubali kuishi maisha yake na jinsi alivyo.

 Amou Haji ni mzee kutoka Iran ambae hajagusa maji kwa zaidi ya miaka 60,Kwa tafsiri rahisi hajawahi kuoga kwa zaidi ya miaka 60. Mzee huyo kwake yeye anaamini kuoga kuwa safi kutamfanya aumwe hivyo kuepuka kuumwa hataki kukugusa maji kabisa.

 SOMA PIA:IFAHAMU APP YA KUSOMA HADITHI KWA KISWAHILI

Mara nyingi hutulia na kuvuta kiko yake ambayo huweka mavi ya wanyama badala ya Tumbaku kama ilivyozoeleka. Mr Haji ambae kwa sasa ana miaka 83 anasema aliamua kuishi maisha hayo hasa baada ya kupata misuko suko kadhaa ya kimaisha akiwa kijana hali iliyompelekea kuamua kuanza kuishi maisha hayo.
Kiko yake ikiwa imewekwa kinyesi cha wanyama badala ya tumbaku
Maskani yake yapo katika Kijiji kinachofahamika kwa jina La Dejgah,Kusini mwa jimbo la Farsi huko Iran ambapo Usiku wake yeye hulala katika shimo ambalo lipo kama mfumo kama wa Pango na muda mwingine hulala katika kajumba kadogo ka mawe ambako wanakijiji walimjengea iliaweze kujihifadhi.

SOMA PIA>>IFAHAMU HAPA TECNO PHANTOM 8 SIMU KALI KWA PICHA

Inasemekana baadhi ya Vijana walimdaka ili kumuogesha lakini alipata upenyo wa kutoroka ambapo alikimbia na kuwashinda mbio vijana hao.
Ukiachana na suala kuoga pia jamaa,Hata kwenye misosi anapenda misosi michafu chafu mfano anasema kwake anapenda Nyama ambayo imeoza na pia anapenda kunywa maji kutokea dumu chafu,
Lakini usifikiri Mzee huwa hajitazami,Ana kioo chake ambapo hujitazama kila mara ili kucheki muonekano wake na pia pale anapotaka kukata nywele zake huwa anaunguza mawe katika moto na kutumia hayo katika kukata nywele zake.

SOMA PIA:WAFAHAMU WAIGIZAJI WAKUBWA AMBAO NI MASHOGA

Kuhusu nguo,anavaa nguo zilizounga unga na kipindi cha baridi hujiongeza na nguo zaidi

Rekodi ya mtu ambae hajaoga kwa muda mrefu inashikiliwa na mzee kutoka India ambae hajaoga kwa zaidi ya miaka 40,Akifahamika kwa jina Kailash Singh Ambapo yeye anadai hiyo rekodi tayari ameivunja.

Chanzo:Dailymail pamoja na Picha 

TAZAMA BAADHI YA PICHA ZAKE HAPA CHINI, 





No comments:

Post a Comment

Pages