Pamoja na visanga vyote hivyo Biggie hakutoa diss
Track kujibu mapigo wala hakujibu lolote juu ya kile kilichoendelea aliendelea
na mishe zake kama kawaida mpaka baadae alipokuja kuachia ngoma “Who shot ya” na
hii aliichia baada ya kifo cha Tupac.
Endelea……………..
Ukimya wa Biggie juu ya beef hii uliwashtua wengi
hasa mashabiki zake wakawa wanajiuliza kwa nini Biggie hamjibu Tupac? Kwa nini
amekuwa kimya? Haoni kama hii itaathiri kazi zake kwani anashambuliwa bila yeye
kurudisha mashambulizi? Hayo yalikuwa maswali waliokuwa wakijiuliza mashabiki
wa Biggie. Pamoja na kutoonyesha reaction yoyote bado hili beef limebaki kwenye
historia ya game ya hip hop duniani.
Kwa kuwa Tupac aliuawa mwaka mmoja kabla ya Biggie,
hivyo Biggie alitumia muda huo kuziba mianya aliyoachiwa na Tupac kwenye kazi
zake . Kwa upande wangu pia ukiniuliza ni nani alishinda kwenye beef hii
nitakujibu ni Tupac kwani jina la Tupac limeenea maeneo mengi duniani na pia
amewahamasisha vijana wengi kwenye game ya rap ukilinganisha na Biggie na pia
muziki wake unajulikana sana ukilinganisha na kazi za Biggie hivyo kwa upande
wangu pia nithubutu kusema Tupac alishinda kwenye beef hii.
BIG Notorious |
Swali lililopo vichwani mwa watu ni nani alimuua
Tupac?
Zipo nadharia(Theories) nyingi juu ya kifo cha Tupac
, ukumbuke Tupac ni mmoja ya wasanii waliouza sana sokoni, ameuza jumla ya
rekodi 75 million, bila kusahau baadhi ya movie ambazo ali act na kuweka
heshima kwenye jamii ya rap.
Tupac alipigwa risasi tareh 7 September 1996 huko
Las Vegas Nevada baada ya mechi kati ya Mike Tyson na Bruce Seldon, Baada ya
shambuli hilo alichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Tiba
kwa ajili ya matibabu.
Alifanyiwa upasuaji kadhaa lakini kutokana na moyo
wake kuathirika kwa kiasi kikubwa siku sita mbeleni yaani tarehe 13 September
aliaga dunia.
Itaendelea…………
Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv