Wengi tunapenda kusikiliza Nyimbo mbalimbali na kuwapa sifa za
kumwaga Wasanii na kuwasahau watu ambao pengine huwa na Mchango mkubwa kuzidi
hata Msanii mwenyewe.
Kutana na Mtayarishaji wa Muziki ambae katika Muziki ameanza
kufahamika siku za karibuni lakini kwa kazi aliyofanya mpaka sasa unaweza
kusema alikuwepo katika Kiwanda cha Burudani kwa kipindi kirefu.
Mwandishi wetu, Alifanya mahojiano na mtayarishaji wa Muziki matata,
S2KIZZY ambae anapatikana katika Studio ya Switch Records, Ambayo inamilikiwa
na Msanii Quick Racka.
Wapi
Ametokea?
Anafunguka kuwa safari yake ya Muziki ilianza tangu akiwa
Shule Ya Msingi,Kiwira Coal Mining ambapo anasema alikuwa akipenda kuimba na
pia kupiga ngoma na mambo mengine ya kiburudani.
“Nilikuwa napiga ngoma watu walikuwa wanapenda sana, na pia
nilipomaliza Shule Ya Msingi nilianza kufuatilia mitandaoni namna watu
mbalimbali wanavyotengeneza mabiti sababu tayari nilianza kuona kama ninaweza
kufanya hicho kitu,”
“Mimi sijawahi kufundishwa kuandaa nyimbo, nilikuwa
najifundisha mwenyewe kwa kuangalia namna watu mbalimbali wanafanya, Nashukuru
sana kwa sapoti kwa Mwalimu wangu mkuu wa Shule ambae alikuwa na Studio ambayo
mara kwa mara nilikuwa ninakaa pale na kujifunza,”
Ngoma
kali zake anazozielewa.
Anasema kuwa mpaka sasa amefanya ngoma nyingi sana na Wasanii
tofauti lakini mpaka sasa ngoma kama Rich Mavoko aliyomshirikisha Patoranking-
Rudi, Country Boy aliyomshirikisha Mwana Fa-Turn Up na pia Country Boy-Ahaa
Wapi ndizo anazozikubali zaidi na kuziheshimu.
“Ngoma ya kwanza kunipa zaidi mafanikio ni Ahaa Wapi ambayo
nilifanya na Country Boy naiheshimu sana na pia hata ngoma zingine kam Jay Mo
ngoma ya Me And You zipo nyingi sana ila hizo naziheshimu sana,” aliongeza
Nae pia
kumbe ni Msanii.
Anafunguka zaidi kuwa watu pia wajue kuwa yeye pia ni Msanii
lakini anasubiri wakati sahihi wa kuachia wimbo wake.
“Mpaka sasa nina Albamu kama nne hivi nasubiri wakati sahihi
ili namimi nianze kuachia Nyimbo kama msanii na sio mtayarishaji wa Muziki
pekee,”
Anamzungumziaje
Country Boy?
“Yani kiufupi jamaa ana mchango mkubwa sana kwangu, sababu
ndio mtu wa kwanza kuniamini na kufanya kazi na mimi, na baada ya kufanya nae
kazi tu nilianza kuona njia nyingi zimeanza kufunguka mpaka sasa nipo hapa,”
anasema
Kuhusu
kazi za Kimataifa.
Anasema mpaka sasa kafanya kazi na wasanii wakubwa Afrika,
kama Casper Nyovest,Nasty C, Patoranking pamoja na wasanii wengine.
SOMA PIA: ZILE SERIES ZOTE KALI ZIPO HAPA
“Hizo ngoma naimani kwa mwaka 2018 zinaweza kuachiwa kwahiyo
tuendelee kusubiri watu wazidi kuona ufundi wangu mwingine nje kidogo ya
Bongo,”
Mtayarishaji
(Produza) Anaemkubali sana.
“Mimi namkubali sana
Nahreel, tangu muda sana nilikuwa namuangalia na kuna mengi nimejifunza
kutoka kwake ila ndio mtayarishaji wangu ninaependa sana kazi zake,” anasema
Pesa yake
ya kwanza alifanyia nini
“Pesa yangu ya kwanza aisee sikumbuki fresh kwa sababu pesa za
utayarishaji mimi nimeanza kupata tangu nikiwa nasoma ila nakumbuka kwa
asilimia kubwa nilikuwa nazitumia kununua vifaa mbalimbali vya Studio kama
Headphones,Mics na vifaa vingine,”
“Ila mpaka sasa nashukuru Mungu Pesa kadhaa nilizopata
nimeziingiza katika mambo mengine ya kibiashara zaidi si unajua tena hizi kazi
zetu,” anaongeza
No comments:
Post a Comment