Maoni Yangu Kuhusu Wonder Woman#Uchambuzi - teknomovies
Maoni Yangu Kuhusu Wonder Woman#Uchambuzi

Maoni Yangu Kuhusu Wonder Woman#Uchambuzi

Share This
Jana Niliamua kuchukua muda wangu mzuri kutazama movie hiyo unayoiona kwenye Picha hapo. 

Na Haya ni mambo machache ambayo wakati nikiwa natazama niliyaona, binafsi movie ninapo itazama huwa nakua na mambo mengi ninayo yatazama.

Hii movie ukitizama hata uwe unafanya michezo mengine sijui, utaelewa tu maana sio Story ngumu saana na hii ni kwa movies nyingi za SuperHeroes...au movies za Science Fiction nyingi hazinaga Ugumu ugumu katika kuzielewa.

Utachopenda nami Nimependa Designing ya Ndani, by tha way Mchongo setting yake imewekwa Kua ni miaka ya vita ya kwanza ya Dunia, na katika hilo Costume designing Yao Imekaa Vizuri.

Ufundi wa VFX na CGI katika hilo wazungu huwa wanatisha sana, But Hii Movie Imepata Sifa Kedekede, lakini kwangu kama kuipa rating ningeipa 5 ya 10 Yote Kwa Upande Wangu....

Kwa sababu, movie hii ya kitoto saana yani mtu mzima kama Mimi Ninapotazama Sikupata hisia kama nipo natazama movie ambayo nilikua naisubiria kwa hamu.

Kingine Uongo kama Kawa Humu, Ni uongo wa karne, Ila Sio mbaya maana ukiwa unatazama movie yoyote Ya Science Fiction.. Ushaona Neno Fiction... Basi Humo Ni Uongo Tu.

Kingine mimi Binafsi Tu Sijaipenda, Ila Sio Kwamba movie hii mbovu... Hapana nzuri sana, na ndomana imepata mauzo makubwa sana na ratings kubwa kuna Action Perfomances nzuri sana sana,na Hata Waigizaji Wamefanya Kazi Safi Saana.

PITA HAPA PIA>>PAKUA HAPA WONDER WOMAN

Toka IMDB imepata rating ya ya 8/10 na Rotten Tomatoes imepata Rating ya 92% na Upate Wa Google Rating imesoma 92% na kumbuka hizo rates zinakuja, kutokana na mjumuisho wa Ratings za watu wanaopiga kura kupitia mitandao hiyo baadae ndo mjumuisho hufanywa.

Na mauzo mpaka sasa ni $720M toka Budget $149M so hapo nazani umeona faida ambayo movie imetengeneza hiyo ni mojawapo ya kiashiria kwamba movie ilikua inasubiria kwa hamu, na imefikia mategemeo ya watu.

Kuna jambo ila pia Nilipenda, ni kuhusiana na Soundtracks za ndani zipo Vizuri.. Kuna wimbo mmoja Kaimba Sia kama sikosei unaitwa Humanity. Linapigwa mwisho hivi, wakati movie inapoisha.

Record baadhi ilizoweka hii movie mpaka sasa ni Movie pekee ambayo imeuza sana huku ikiwa imeongozwa na Mwanamke ambaye Anafahamika kwa jina la Patty Jenkins pia ikiwa movie  iliyouza zaidi kwa nyumbani marekani katika week za mwanzo za ufunguzi na rekodi nyingine ikiwa movie iliyouza zaidi ikiwa imechezwa na mwanamke as Super Hero.

Nawe pia unaweza ukaacha maoni yako hapo kwenye kisanduku cha Comment Kama umetazama hii movie, ukatoa maoni yako pia. 

Pages