Spider Man Homecoming, Yatazamiwa Kufanya Vizuri. - teknomovies
Spider Man Homecoming, Yatazamiwa Kufanya Vizuri.

Spider Man Homecoming, Yatazamiwa Kufanya Vizuri.

Share This
Dogo baada ya kupewa mchongo katika vita ya SuperHeroes (Avengers) anatamani zaidi na zaidi kupata mission nyingine zaidi, Lakini Tony Stalk a.k.a Iron man ambaye ndiye aliyemwita Dogo katika team yake anamwambia kua inabidi asubiri mpaka atakapopigiwa simu na anampa ushauri kwa muda huo inabidi abaki kua mtu mzuri kwa watu wote na majirani pia. 

Tony anampa no ya Security Guard Wake Happy Hogan.. Lakini Peter kila akipiga simu na kutuma texts, Hajibiwi hivyo anabaki tu akiwa katulia tuli akiendelea kusubiria simu kutoka kwa Tony kumpa miongozo mingine.

Tony aliamua kufanya sababu kwanza dogo kuna mengi ilibidi ajifunze toka mazingira anayoishi yote sababu bado dogo ana umri wa miaka 15,hivyo kumpa majukumu mazito ni jambo lisilo ba busara kwa manufaa yake.

Lakini hali inabadilika baada ya hali ya hatari kutokea, tokea kiumbe cha ajabu ambacho kinafanya uharibifu na mauaji Kwa watu.

Peter anaamua kuanza kufanya kazi hivyo hivyo ya kuokoa maisha ya watu bila kupata ruhusa toka kwa Tony.

Jambo ambalo tunalisubiri kwa hamu toka hii movie ni kumuona mtu ambaye atacheza kama Villain ( Jambazi Kuu) na pia ushirikiano kati ya Tony na Peter katika kuchangamsha movie itakuaje.

Tunaendelea kuhesabu masaa tu mpaka sasa, kabla ya huu mchongo kuoneshwa Mubashara katika makumbi ya Cinema mbalimbali duniani.

Ni filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu sana ukilinganisha hii itakua tofauti kidogo na zilizowahi kutangulia kutoka na mpaka sasa, filamu hii imelamba Rates za juu toka mitandao mbalimbali kama na sasa kinachosubiriwa ni kuona mafanikio ya kimauzo zaidi na zaidi.



Pages