Bidhaa kutoka kampuni ya Apple si ngeni machoni mwetu aidha kwa kuzitumia,kuzishika au hata kwa kuzisikia. Apple ni kampuni ya Tarakilishi (Computer) iliyoanzishwa mwaka 1976 na watu watatu ambao ni Steve Jobs, Steve Wozniak na Ronald Wayne.
Mwaka 2016 Kampuni hii ilitimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake sasa yapo ambayo pengine huyafahamu kutoka kwenye kampuni ya Apple, mtandao wako Pendwa wa teknomovies.com umekuandalia machache kuhusu kampuni ya Apple.
1. Ronald Wayne ambae ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple aliuza hisa zake za Apple kwa dola 800 za kimarekani muda mfupi tu baada ya yeye na wenzie kuanzisha kampuni hiyo. Inasemekana kwamba alifanya hivyo baada ya kuhofia kwamba iwapo Apple wangeshindwa kibiashara basi mali zake zingebinafsishwa.
Wasichojua wengi kuhusu Ronald Wayne ni kwamba anajihusisha na mahusiano ya jinsia moja na alimwambia habari hii Steve Jobs wakati bado wakiwa waajiriwa kabla hawajaanzisha kampuni ya Apple. Ronald anasema hajutii kuuza hisa zake wiki chache baada ya kuanzishwa, anadai kwamba alifanya maamuzi hayo kwa kutegemea taarifa aliyokuwa nayo kipindi kile. Yeye ndie mbunifu wa logo ya kwanza ya Apple.
Ronald Wayne |
2. Steve Jobs aliuza gari lake ili aweze kutengeneza kompyuta ya kwanza ya Apple
Pesa ambazo ziligharamia utengenezwaji wa Komptyuta ya kwanza ya Apple ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la Apple Computer 1 ama Apple 1 zilitokana na pesa zilizokusanywa baada ya Steve Jobs kuuza usafiri wake wa pekee wa VW Mini Bus na Steve Wozniak kuuza calculator yake ya HP-65.
Jobs aliuza gari lake la pekee ili kulipa gharama za kutengeneza kompyuta ya kwanza. Gari hilo lilikuwa kama hili.
3. Kompyuta ya kwanza ya Apple ilichukua siku kumi tu
Kompyuta ya kwanza ya Apple |
4. Steve Jobs aliwahi kushushwa Cheo akaamua kwenda kuanzisha kampuni nyingine.
Mwaka 1985 Steve Jobs alishushwa cheo cha umeneja na bodi ya wakurugenzi baada ya kutokea kugombea madaraka kati yake na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa wakati huo. Jobs akaondoka na baadhi ya wafanyakazi wakaanzisha kampuni ya NEXT.
5. Apple walishawahi kuwa na pesa nyingi kushinda serikali ya Marekani
Kwa kipindi cha mwaka 2011 Apple walikuwa wanahifadhi pesa kubwa kushinda hifadhi ya pesa za serikali ya Marekani, hii ilitokana na hasa na ukubwa wa madeni ya Marekani kwa wakati huo.
Bonus
Nakuongezea na hili. Ukiangalia kwa makini kwenye logo ya Apple kuna sura ya Steve Jobs.
Yako mambo mengi ambayo hayajulikani kwa watu hasa watumiaji wa bidhaa za Apple hayo matano ni machache ambayo mimi nimepata kuyafahamu.
No comments:
Post a Comment