Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi NeNO Kwa Neno - teknomovies
Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi NeNO Kwa Neno

Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi NeNO Kwa Neno

Share This
Katika Hip Hop wanasema ndo sehemu pekee ambayo kwa asilimia kubwa unaweza kutoa ya moyoni yako alafu ikawa Fresh kama Fid Q.

October 10 katika usiku wa utoaji tuzo za BET Hip Hop Awards,Eminem aliachia Cypher yake kali ambayo alimchana sana Rais Donald Trump na kuungana na mahasimu wakuu wa Trump kwa upande wa wasanii kama Snoop Dogg ambae yeye aliachia kabisa jiwe ambalo lilimdiss Trump.

Trump nae pia alitumia Twitter yake kumjibu Snoop Dogg hali iliyozidi kuleta utamu flani alafu wa ajabu kwa namna Rais Jinsi anavyojiingiza kwenye mambo ambayo watu wanasema ya kijinga.

By tha way,Mimi naachana na hizo blah blah,Lengo langu ni kuchambua Mistari ya Eminem ili watu waelewe vizuri.

Katika Cypher hiyo,Eminem hajatumia biti lolote hivyo sauti yake inasikika vyema kabisa ni wewe kutega sikio lako vizuri tu.

Huo ni mwanzo ambapo Eminem anasema kuwa,Mwanzo ilikuwa ni fresh kabla ya gharika kuingia akimaanisha kuwa mwanzoni ambapo ulikuwa ni utawala wa Obama hali ilikuwa safi lakini kwa sasa ni gharika baada ya utawala wa Trump kuingia, alafu anajiuliza tena mwenyewe namna ambavyo ataanza michano yake..kama kawaida yake,Akisemega hivyo kwa wanaomfahamu wanajuaga kinachofuata ni mazishi.


Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza Eminem anatuambia  kwa kutuoneshea sisi mashabiki kwamba kama nijivae u Eminem namnukuu “jamani mmeona hicho kikombe cha kahawa cha moto vibaya mno,vipi si nimwagie tu Donald Trump? lakini kiukweli sitofanya hivyo lakini nitachofanya kwa Trump huyu ni kumpiga kwa maneno tu yanayoeleweka na tena nina mpango na sasa hivi kwenda kufanya.... hapo akataja neno Apache ambao ni mtaa flani huko Paris ambao ni hatari sana,yani mpaka polisi huko wanaogopa kutimba maana ni vurugu sana,Lakini kwa maana nyingine ya neno hilo mtaa wowote ule ambao ni hatari kwa mambo tajwa,unaweza kutumia hilo neno.

Kwahiyo yeye Eminem atachomfanya ni kama mtu ambae ametoka katika mitaa ya namna hiyo,alafu kashika kisu kikali sana..huo moto wake unakuwa ni balaa sababu ya matukio kadhaa ambayo huwa yanatokea huko mengi huwa ni ya kushambuliwa na kisu.

Tena anaongeza hapo,kwamba baada ya kushika hicho kisu... ataingia msikitini mwezi wa Ramazani na kuomba kwa Allah kila kitu ambacho Melania ambae ni mke wa Trump huwa anaongea.

Zaidi Eminem anazidi kusisitiza kuwa inabidi Waendelee kumpa heshima sana Obama , na yote kwa sababu safari hii ambae yupo Ofisini anachokifanya ni kama anawalipua na makombora ya hatari akitumia neno “Kamikaze” ambalo ni neno kwa asili lililotokea katika vita ya pili zikipewa jina za ndege za kijapani ambazo zilikuwa zinabeba makombora mazito na kwenda kuachia katika tageti maalumu na zilikuwa zikileta athari kubwa,hivyo jamaa kamfananisha kama ndege hizo katika nchi ya Marekani na kwamba Jamani Wamarekani wenzangu huyu Mshikaji wetu (Trump) Yupo kutuua kama ndege hizo zilivyokuwa zinafanya ambapo kama unakumbuka katika vita ya pili ya Dunia Wamrekani walipigana na Japan,Na wanajeshi wengi sana wa Kimarekani walipoteza maisha hasa Kutokana na Mashambulizi hayo……oooops Serious Eminem? Yani Trump ndo anachowafanyia??


Tutaendelea…..

Bonyeza Chini Hapo Play Kutazama Kama Bado.

              
Usisahau Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Update mbalimbali lakini pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.

Pages