Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi Neno Kwa Neno Part 02 - teknomovies
Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi Neno Kwa Neno Part 02

Matusi Ya Eminem Kwa Trump,Uchambuzi Neno Kwa Neno Part 02

Share This


Yeah..Eminem anaendelea zaidi kumponda Trump,Sikia Lines kama hizi anakwambia..


Eminem anaendelea kuwa wakati blah blah zinazidi kuendelea yeye Trump amekaa tu akisubiri eti kwamba mambo yakae sawa kivipi sasa?Kwa maana kwamba kelele nyingi za Trump huwa sio za kutibu bali ni kama zinachochea zaidi  na hapo Eminem kamfananisha na mtu ambae anakaa akisubiria mambo kuwa sawa bila kufanya jambo lolote lile,Kamwe huwezi.

Na zaidi anaongeza kuwa,Huyu Trump mambo yakija kuchafuka yeye atachofanya ni kuweka ndege yake mafuta na kupaa angani na akisubiri kushuka mpaka huku chini mabomu yatulie wakati tushachafuana vya kutosha….kwa maana zaidi ni kuwa jamaa huwa anaongea sana kauli ambazo zinakaribisha vita.

Wakati huo hajali wananchi as we know kwamba siku zote vita mtu anaeteseka ni mwananchi na si viongozi.

Anaongeza zaidi kuwa Trump kwenye suala la kuongea Pumba yani uko vyema kama Mimi tu (Yeye Eminem) lakini tofauti yangu na wewe ni kuwa pale unapokuwa na mpira ili uje unikwepe (Mfano kama wa mpira wao wanaita Rugby) wewe unachofanya ni kuficha….hahah hapo tafsiri ni kuwa Eminem yeye ukimzingua na yeye anakuzingua lakini Trump ukimzingua anapiga blah blah sana na si kufanya the same. Daah weee Eminem weee..

Kama kawa Eminem hakuacha kusema suala zima la ubaguzi ambalo mara kadhaa Trump amekuwa akisemwa ambapo anasema kwa Trump yani ishu kwake ambayo yupo fresh yani ni kwenye Ubaguzi tu.

Racism's the only thing he's fantastic for……Eminem anaongeza zaidi kuwa sababu kuu ambayo hawamuogopi Trump ni kuwa,Trump yeye anatembea kwenye maganda ya mayai afu Eminem katokea sehemu za hatari kwenye makelele kwahiyo atamueleza nini kwa mfano?..Tafsiri ya mtu kutembea kwenye maganda ya mayai ni kama unamfananisha kuwa ni bishoo tu yani Trump maisha yake yote amepitia maisha ya kidoni…alafu Eminem katokea uswazi sasa utamueleza nini kuhusu maisha kwa ujumla?

Tena anaongeza kuwa jamaa kutokana na maisha aliyopitia ndio maana anapiga kelele kuwa mabwawa wayafungulie maji na yote sababu lenyewe lipo kwenye mchanga safi…tafsiri ni sawa kama unamwambia mtu asitumie mkaa alafu huku unapandisha bei ya gesi unategemea nini kwa mfano? Si kuuwa kimya kimya huko.

Tazama lines hizi anakwambia “It's like we take a step forwards, then backwards
But this is his form of distraction
Plus, he gets an enormous reaction
When he attacks the NFL so we focus on that in,"

Anakwambia kwa uongozi wa Trump ni kama tunaenda mbele hatua kadhaa alafu tunarudi tena  nyuma hatua zile zile hahaha mwendo wa kilevi au sio ,lakini Eminem ashangai sana kwasababu mtu aliyepo madarakani hajali kitu…kingine anaongeza kuwa anashangaa kwa jinsi anavyojibu mambo mfano akatolea ishu ya wanamichezo kadhaa wa Nfl ambao waligoma kuimba wimbo wa taifa na trump kwenda kuwaatack katika mtandao wake wa Twitter…sasa kile kitendo Eminem anasema jamaa linaaribu mambo afu linafanya hivyo ili akili zetu tuziweke huko..tumemshtukia.

Eminem kama kagusa vingi sana ,mfano ishu ya Puerto Rico ambapo Trump alitoa kauli kwamba watu wa huko baada ya kukumbwa na kimbunga na wengi kupoteza maisha na pia makazi yao kuharibiwa wamekuwa dizaini wavivu wanataka kila kitu wafanyiwe na Marekani..na pia Trump ishu ya Nevada kuhusu masuala ya umiliki wa silaha,,sasa Eminem anamwambia Trump kuwa badala ya kuongea kiukarimu na kutatua mambo kama hayo wewe unaongea Pumba tu Twitter, alafu unatuambia eti utapunguza Kodi,sasa unafikiri nani yupo tayari kukulipia safari zako hizo za anasa,unazoamua kwenda na kurudi alafu unaenda kutulia kwenye viwanja vya gofu na kwenye maeneo yako ya kujitanua soma lines hizi 

stead of talkin' Puerto Rico or gun reform for Nevada
All these horrible tragedies and he's bored and would rather
Cause a Twitter storm with the Packers

Then says he wants to lower our taxes
Then who's gonna pay for his extravagant trips
Back and forth with his fam to his golf resorts and his mansions?

Tutaendelea...


Pages