Suge hakupenda label yake ishiriki kwenye mambo haya
kwani walikuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye misaada lakini
alishindwa kumwambia Tupac juu ya suala hilo kwani yeye ndo anaeleta faida
kubwa kwenye label yake sasa akimwambia si atavuruga biashara? Ikabidi avumilie
tu na ashiriki kishingo upande. Kikubwa kilichomuumiza ni siku waliyotumia
takribani $ 60 million kwa ajili ya msaada, hili Suge lilimuuma mno.
Endelea…………
Tupac aliskwishajua mahusiano yake na Suge hayana
muda mrefu yatavunjika hii ni kwa sababu yale anayoyafanya hayampendezi
mwenzake kwani Suge akili yake ilikuwa kwenye pesa tu na si kingine hivyo tupac
akaamua kuanzisha record label yake ya Makaveli ambayo aliitumia kusambaza kazi zake na baadae akamsainisha
moja ya wasanii wa rap “The Outlawz”.
Wakati Tupac anaanzisha record label , Suge alijua Makaveli Records itakuja kuwa
na mafanikio, hilo lilimshtua kwani aliona kila dalili ya record label hiyo
kuwa tishio upande wa West (West Coast Side). Alichokuwa anakifanya Tupac ni
kuiba baadhi ya wasanii kutoka katika label ya Death Row na kuwavuta Makaveli
Record na kuna nyakati Suge uvumilivu ulimshinda akawa anamchana Tupac.
Suge aliogopa umaarufu wa label ya Makaveli utamvurugia
Biashara ya label yake na mwisho wa siku apotee kwenye ramani ya muziki hivyo
hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kumpoteza (kumuua) .
Ukumbuke Tupac tayari ana beef na Biggie, P Diddy
katika ishu za muziki na polisi nao walikuwa hawampendi Tupac kutokana na tabia
zake za awali ambazo zilikuwa si za kistaarabu hapo nyuma ingawa alibadilika
lakini ndo hivyo tabia ni kama ngozi ya mwili.
Kutokana na nadharia hizo Suge alijua kabisa tukio
la mauaji likifanyika basi watakaonyooshewa vidole ni wengi kwani Tupac
alishajiweka kwenye mazingira ya beef na watu wengi, sasa ili asijitenge kabisa
akaanza kuwa karibu na Biggie kwa kusapoti nyimbo zake lakini pia akawa karibu
na polisi ili asibaki kuwa na uapnde wake bali awepo pande zote.
Tarehe 7 September 1996 siku hii kulikuwa mechi ya
ndondi kati ya Mike Tyson na Bruce Seldon ambayo ilifanyika huko Las Vegas
Nevada, kwa kuwa Suge alijua Tupac na Tyson ni marafiki basi kivyovyote vile
ataenda kwenye mechi hiyo, hivyo na yeye akaamua aende na awe upande huo huo wa
Tyson. Siku hiyo Tupac alikuwa na show kwenye club ya Suge’s night club “662” akasita kwenda Vegas kwa ajili ya
kutazama ndondi lakini baadae alikubali .
Siku hiyo
pia Bodyguard wake alimwambia asibebe Bastola kwani yeye atamlinda huko Vegas
na hii ilikuwa ni mara ya kwanza Bodyguard huyo kumuomba Tupac aache silaha na
kweli Tupac alitii agizo hilo. Wakaenda Vegas kucheki mechi nae Suge alikuwepo
na katika pambano hilo Tyson alishinda katika round ya 10.
Wakati
wanatoka katika ukumbi wa MGM Grand, Tupac aliona mtu akipora cheni kwa mmoja
wa watu waliokuwepo kwenye mechi hiyo, jamaa aliyeporwa hakukubali wakaanza
kuzichapa na hapo Tupac aliamua kuingilia ugomvi huo, kumbe ugomvi huo ulikuwa
ukihusisha vikundi viwili kutoka West Coast Side vikundi hivyo vilijulikana kwa
majina ya Crips na Bloods. Wakati hayo yote yanatokea Suge alikuwa akishuhudia
kwani aliamua kufuatilia kila tukio analofanya tupac usiku huo .
Itaendelea..........
Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali na pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.