Gosby: Rapa Anaeamini Katika Elimu - teknomovies
Gosby: Rapa Anaeamini Katika Elimu

Gosby: Rapa Anaeamini Katika Elimu

Share This
Staili ya Muziki aina ya Trap ambayo imeibuka kwa miaka ya karibuni imeonekana kushika kasi kwa kiasi kikubwa huku Bongo nao wasanii mbalimbali wa Rap wakiifanya japo imekuwa na mapokeo hafifu.

Moja ya wasanii wanaosifika kwa kufanya Trap kali huwezi kuacha jina la msanii Gosby,ambae floo zake pamoja na mashairi yake tangu anatoka mpaka sasa ameweza kujijengea ngome yake.

Alikoanzia.

“Nilianza Muziki tangu nikiwa shule tena nilikuwa naimba kipindi hicho,lakini baadae nilianza kurap na watu wakawa wanapenda zaidi nikiwa narap sababu kwa kipindi hicho nilikuwa nafanya sana remix za wasanii wengine kwenye miaka ya 2007,”

“Wimbo wangu wa kwanza kupata mafanikio ulikuwa ni Everyday ambao niliutoa mwaka 2012 ulipendwa sana na baadae zikaanza kuja zingine ambazo zilifanya poa pia kama BMS,”  aliongeza.

Mgogoro na B Hitz

Kipindi Fulani Gosby alikuwa akifanya kazi zake katika studio za B Hitz ambazo zinamilikiwa Hammy B chini ya produza Pancho Latino ambapo kuna mgogoro ulitokea uliosababisha wasanii waliokuwepo katika lebo hiyo wote kuondoka akiwepo yeye pia.

Akizungumza kwa sasa uhusiano wao anasema kuwa wapo fresh  “Mimi na B Hitz  tuko fresh tofauti na watu wanavyofikiria na hakuna shida yoyote ile yale matatizo yaliyokuwepo mwanzo yalishaisha na maisha yanaendelea,” aliongeza

Mixtape  yake.

“Mixtape yangu inakuja mwezi machi mwakani au pia inaweza kuwahi sababu kuna vitu tupo tunaweka sawa yakiwa sawa tu watu wataanza kuipata maana nasumbuliwa sana,”

Wimbo wake na Izzo B

Kolabo yake na Izzo B inayokwenda kwa jina la Oh No anasema kuwa hakupanga kufanya na Izzo B lakini alikuwa na mipango nae tangu muda ya kufanya nae ngoma.

“Hii ngoma kuna watu walinizingua nilitaka kufanya nao,hivyo nilipodondoka kwa Izzo B yani fasta jamaa akanibariki na mashairi yake kwenye ngoma yangu,” alisema.

Elimu na Muziki.

“Mimi elimu yangu nimeishia chuo na nilianza muziki tangu nikiwa shule na sikuacha shule nimeweza kufanya yote na kwa ubora na kuna mambo naona kabisa elimu inachangia kwa namna muziki wangu ninavyofanya,”

“Nawashauri sana na  bado ntaendelea kuwashauri rapa wengi,kamwe wasijaribu kuacha shule sababu ya muziki nawaambia unaweza kufanya vyote kwa wakati mmoja ni wewe kupanga muda vizuri basi,”

“Kwanza Muziki ukiwa na Elimu kidogo inasaidia sana katika mambo mengi hata uwasilishaji na ujuzi wako unakuwa vizuri sana,”Aliongeza

Kimya kwenye gemu


“Nimekaa kimya kidogo kwenye gemu sababu nilikuwa nafanya mambo mengine ambayo yalikuwa yananibana kuweza kufanya muziki lakini kwa sasa nimeshapanga mambo yangu vizuri na ndio maana nimeachia dude hilo ambalo video yake inakuja baada ya kama wiki mbili,” 

Pages