Ray C ampiga stop Nandy,Kuacha Kutumia Nyimbo Zake - teknomovies
Ray C ampiga stop Nandy,Kuacha Kutumia Nyimbo Zake

Ray C ampiga stop Nandy,Kuacha Kutumia Nyimbo Zake

Share This
Kupitia akaunti yake ya Instagram Mwimbaji Ray C amemchana mwanamuziki mwenzake wa kike Nandy na kumpiga stop kutokutumia nyimbo zake katika kufanya shoo zake ambapo Ray C amedai hii ni kama mara ya pili anafanya hivyo kwa sababu bado hajafa hivyo kama anataka hivyo ni bora amuite.

Jamaani hii tabia sio nzuri kabisa!!! Sijafa bado! Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye show zenu muwe mnaniitaga basi!sina cancer ya koo ya Kushindwa kuziimba hizo nyimbo!Nandy hii mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako! Hii mara ya pili ujue! Mashabiki zangu hamuwatendei haki!i don't like it sipendi! Maana hata tukigongana muda mwingine hata salam bambini kwahiyo staki mazoea.......
"Niliimba tusitaftiane visa tena Pisha sio tena Presha" Ameandika.

Nae Nandy akijibu kuhusiana na hilo ameandika pia katika akaunti yake Instagram na kusema kuwa anamuheshimu sana na kuzikubali kazi zake na hafikirii kama kumuenzi mtu ni mpaka awe amekufa.


Dadaangu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama mmoja wa wasanii waliotufungulia njia ya muziki wetu ulipo. Sitaacha kukuheshimu na kukubali kwa hilo wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lizima uwe umekufa hapana siamini kwenye hilo sis nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri kama ulivyomuenzi Mama Mwanahela kwa nyimbo zake ulizorekodi za mahaba ya dhati na nimezama. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivo imba nyimbo za wengine nyimbo zao kama mwasiti, king kiki, yemi alade na recho,” ameandika


Pages