LUPITA NAE AMWAGA UCHAFU WA BOSS HOLLYWOOD KUMNYANYASA KINGONO - teknomovies
LUPITA NAE AMWAGA UCHAFU WA BOSS HOLLYWOOD KUMNYANYASA KINGONO

LUPITA NAE AMWAGA UCHAFU WA BOSS HOLLYWOOD KUMNYANYASA KINGONO

Share This
Mcheza filamu na mshindi wa tuzo ya Oscar Lupita Nyong’o, raia wa Kenya, amejitokeza kuungana na wacheza filamu wengine kadhaa wanawake waliotoa shutuma za udhalilishaji wa kingono dhidi ya mzalishaji maarufu  wa Hollywood Harvey Weinstein.
Katika Makala iliyochapishwa kwenye gazeti  la New York Times.Nyong’o ameeeleza uamuzi wake wa kusimulia kisa kilichomkuta hivi sasa akiungana na wanawake wengine ambao walikuwa  wamedhalilishwa kimapenzi.
SOMA PIA : BOSI WA AMAZON KITANZINI KWA KASHFA YA NGONO

Nilikuwa nimeweka dukuduku langu dhidi ya Harvey mbali kabisa na akili yangu, na kujiunga na wale waliokubaliana kunyamaza dhidi ya uovu huu ambao umempa nafasi mwindaji huyu wa ngono kuwadhalilisha wanawake kwa miaka mingi. Nilikuwa najihisi niko peke yangu wakati udhalilishaji huu ulipotokea, na nilijilaumu kwa yaliyotokea, kama vile ilivyokuwa kwa wanawake wengine ambao wamesimulia dukuduku lao.

Lakini kwa vile hivi sasa suala hili linazungumziwa kwa uwazi sikuweza kujizuilia na kumbukumbu zangu juu ya udhalilishaji huu zilizojitokeza. Nilijisikia ndani ya tumbo langu kuwa ninaumwa. Nilihisi vile hasira zinavyonipanda ni kitambua kuwa simulizi yangu siyo ya kipekee bali ni sehemu ya mfumo wa kitabia.”

Weinstein inadaiwa kuwa alijaribu kumlazimisha Nyong’o wawe na mahusiano wakati alipojitokeza kwenye usahili katika shindano la filamu katika makazi yake  huko Westport, Connecticut. Wakati huo Nyong'o alikuwa bado ni mwanafunzi wa Sanaa ya kuigiza chuo cha Yale.
Harvey Weinstein“Harvey alinipeleka chumbani kwake na akatangaza kuwa alikuwa anataka kunifanyia massage (kunikanda). Nilidhani kuwa alikuwa anatania hapo awali. Ilikuwa siyo hivyo. Kwa mara ya kwanza tangu nikutane naye nilijihisi siko salama. Nilishtuka kidogo na kufikiria haraka jinsi ya kumuepuka na kuweza kujihami nafsi yangu, kujua hasa sehemu gani mikono yake ilikuwa inataka kushika wakati wote huo.
Muda siyo mrefu alisema anataka kuvua suruali yake. Nilimwambia asifanye hivyo na kuwa itanifanya niwe katika hali ya taharuki… nilifungua mlango na kusimama kwenye kizingiti. Alivaa shati lake na mara nyengine alisema jinsi nilivyokuwa mjeuri. Nilikubaliana naye huku nikicheka na kujaribu kuondokana na hali hiyo kwa usalama.”

Kama Nyong’o anavyoeleza, sehemu ya mafunzo yake ilikuwa ni kujifunza namna ya kukanda(massage) na mazoezi ya viungo, lakini Weinstein amedai vitendo hivyo vilionyesha kuvuka mstari. Baadae, anaeleza jinsi alivyopitia katika mchakato wa kutambua jinsi atavyoweza kulishughulikia suala hili kwa umakini zaidi.

SOMA PIA : BILLBOARD YAKUBALI KUTUMIA VIEWS ZA YOUTUBE KATIKA MAUZO YA KIMUZIKI

“Nilikuwa naingia katika biashara ambayo mahusiano mazuri ni sehemu ya weledi na kwa hivyo kuna kujichanganya sana,”

Nyong’o ameandika kuwa “kwa upole alikataa pendekezo hilo” na kumshangaza Weinstein anaongeza kuwa Weinstein alimwambia kuwa “ hatambui ni fursa gani anaipoteza.
Lakini Baadae aliendelea kupiga hatua katika fani hii ya uigizaji, na baada ya Nyong’o kuwa nyota katika filamu inayoitwa 12 Years a Slave, ambayo alipata tuzo ya Academy, Weinstein alimfuata Nyong’o baada ya tafrija ya sherehe hiyo huko Toronto na kumwambia Nyong’o alikuwa anaona fedheha katika nafsi yake kwa kile alichomtendea na kuahidi kuwa atamheshimu kuanzia hapo. 
“Lakini niliweka ahadi moyoni kwamba sitafanya kazi na Harvey Weinstein milele,” ameongeza Nyong’o.

Na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kukutana pamoja, Nyong’o amesema haraka sana aliamua kukaa nae mbali mtu huyo ambae alikuwa akitumia madaraka yake vibaya.
 
Nyong'o ni mwanamke wa 33 kutoa ushuhuda juu ya matukio ya Boss huyo wa Hollywood.

Usisahau Kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies kwa Updates mbalimbali pia Subscribe Youtube Channel ya DM Online Tv.



Pages