BILLBOARD YAKUBALI KUTUMIA VIEWS ZA YOUTUBE KATIKA MAUZO YA KIMUZIKI - teknomovies
BILLBOARD YAKUBALI KUTUMIA VIEWS ZA YOUTUBE KATIKA MAUZO YA KIMUZIKI

BILLBOARD YAKUBALI KUTUMIA VIEWS ZA YOUTUBE KATIKA MAUZO YA KIMUZIKI

Share This
 Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya muziki,Billboard imekubali kutumia VIEWS za Youtube kama kigezo cha mauzo bora ya Muziki. Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa  HITS Daily Double.


Chati kubwa ya muziki na albums ya Billboard Hot 200 imekubali kuchukua Namba ya watazamaji wa kazi za wasanii kama sehemu na kigezo cha kuonyesha kuwa kazi za msanii zinauza na kitawekwa wakati album inaingia kwenye chati zao.

Mpaka sasa tunasubiri kuona wasanii wa nje watapokeaje hili swala ukizingatia wengi hufanya vizuri sana kwenye Youtube kwa video zao na albums kusikilizwa sana.

Hapa YouTube itasaidia kuongeza namba kubwa ya mauzo ya muziki, kupunguza pesa nyingi wanazotumia wasanii kutangaza kazi zao.

Pia wakongwe wa muziki Marekani hawapendi jambo hili na tayari mmiliki wa lebo inayosimamia kazi za Kendrick Lamar  Top Dawg Entertainment CEO Anthony “Top Dawg” Tiffith alisema February 2016, hatupendi wanachofanya Recording Industry Association of America kuhesabu namba za watu waliosikiliza album mtandaoni ‘TIDAL, SPOTIFY’ kama sehemu ya mauzo, tupaki kwenye kununua album kama kigezo, uza album milioni moja , hapo nipehongera yangu.

Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies na pia usisahau ku Subscribe Youtube Channel ya DM Online TV.

Pages