Mwanamuziki Diamond Platnumz amepelekewa wito wa kuitwa Mahakama ya
Watoto na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto kwa madai ya kushindwa kumuomba
radhi na kutoa matunzo ya mtoto.
Wito huo wa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mabetto, Abdullah Zulu
na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Diamond Platnumz anadaiwa kumdhalilisha na kutompa matumizi ya mtoto kwa takribani miezi miwili.
Wakili Zulu akizungumza na Gazeti la Mwananchi leo Alhamisi amesema
mteja wao Hamisa Mobetto alimtumia Diamond notisi ya kumuomba radhi na
kumtaka apeleke matunzo ya mtoto ndani ya siku saba.
“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande
wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi)
tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo
ameipokea,” amesema.
Zulu amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu.
Mhariri Pia Mwandishi Mkuu Katika Tovuti Hii, Usiache Kupitia Kila Siku Kwa Habari Moto Moto.