Diamond na Zari Filamu ndo Kwanza inaanza - teknomovies
Diamond  na Zari Filamu ndo Kwanza inaanza

Diamond na Zari Filamu ndo Kwanza inaanza

Share This
BADO ishu inaendelea kuwa tata kwa upande wa mahusiano ya Diamond Platnumz na Zari ambapo vijembe kadhaa vimekuwa vikitupwa katika kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuzidi kuleta hali ya sintofahamu.

Kesho Diamond anapiga shoo kampala ambapo taarifa zinasemekana kuwa Zari nae angekuwepo ili kumpa sapoti kipenzi chake huyo ambae yupo katika nchi yake alikozaliwa yeye,lakini cha ajabu Zari kupitia akaunti yake ya Twitter amekanusha suala hilo.

Unfortunately I will not be attending the Kampala charity festival as advertised by some blogs due to personal commitments hope u enjoy,” aliandika katika Twitter.

Katika kurasa ya Instagram nae Diamond aliachia povu zito kuwaendea watu wote ambao wamekuwa wakifuatilia maisha yake na kusema kuwa kama akiachana na Zari basi atasema wazi ili watu waache kuongea.

“Mara Diamond Kamla Huyu, mara sjui naskia anatembea na Huyu, Mara Ooh sjui inasemakana juzi alikuwa na Huyu...Yani kila Ukiamka limezuka jipya, Utazani yangu ina Sukari au Nakojoa dhahabu😏.....Hebu Niacheni kidogo, niko Busy nahangaika kuipeleka Bongo fleva yetu Duniani.... Sijamkaza yoyote, na Sina Mahusiano na Yoyote anaetajwa, na Siku pia Nikimaliza Mahusiano yangu na Alie South na nikawa na Mwengine na ikifikia kuliweka wazi ntaliweka wazi Mwenyewe, Maana hakuna kitachonizuia... ndio kwanza nna miaka 28, Sijaoa na Hata nikioa Naruhusiwa niwe na wake Wanne PERIOD,” aliandika

Enzi Hizo Naitwa Domo skuizi Eti Lips Denda Lord have Mercy,” aliongeza katika post nyingine.

Nae Zari kuoneshwa  kukerwa na drama zinazoendelea kupitia kurasa yake ya snapchat aliponda watu wanao ongea kuhusu maisha yake binafsi kuwa wamuache.

Ati nini? Yule wa wapi? Hana gina ati Mama T. unachako huku.Can I be left out of this drama please.Naomba,” aliandika

Bado filamu ya wawili hawa imebaki haieleweki huku kukiwa na tetesi kuwa hawapo sawa tena na wengine wakisema mapenzi yao yameshaota mbawa. Lakini kitu kikubwa watu wanasubiri kuona namna shoo ya Kampala ya Diamond itavyokuwa na kwa namna ipi atapokelewa Uganda?

Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa Diamond kufanya shoo Uganda,lakini mara ya mwisho kufanya shoo huko ni kipindi ambacho alikuwa vizuri katika mahusiano yake na Zari ambapo alipokelewa kwa shangwe kubwa huku nae Zari akimpa sapoti mpenzi wake huyo.

Pages