SABABU ZILIZOPELEKEA PAUL KUJIENGUA KATIKA KUNDI LA P SQUARE - teknomovies
SABABU ZILIZOPELEKEA PAUL KUJIENGUA KATIKA KUNDI LA P SQUARE

SABABU ZILIZOPELEKEA PAUL KUJIENGUA KATIKA KUNDI LA P SQUARE

Share This
Taarifa za kuvunjika kwa kundi la P Square ziligonga vichwa vya habari kwenye vyombo mbalimbali kuanzia mwaka 2016. Katika kipindi hicho Paul alikuwa tayari ameshaanza kufanya kazi zake kama msanii wa kujitegemea "Solo Artist".

Sasa taarifa ikufikie rasmi kuwa Paul hayupo tena katika kundi hilo la P Square linaloundwa na ndugu zake ambao ni Peter na Jude (Kaka yao).


Katika mahojiano maalum wa mtandao wa burudacni nchini Nigeria Paul amesema kuwa anataka kufanya kitu ambacho anaona ni sahihi kwake na si vinginevyo.

"Nataka kufanya jambo ninalopenda mimi binafsi na si linalopendwa na watu wengine, Unaelewa kampuni inapokuwa na CEO's wengi, hivyo nataka nifanye vitu mimi mwenyewe".

"Muziki si kwa ajili ya maisha ila unawaweka watu karibu pale mnapofanya, lakini narudia kusema mnapokuwa na kampuni yenye mabosi zaidi ya wawili au watatu kuna taratibu nyingi za kufuata nikiwa na record label yangu itakuwa rahisi kutatua changamoto, nikifanya makosa ni mimi mwenyewe na nikifanya mazuri ni mimi mwenyewe".


Usisahau kutufollow Instagram na Twitter @Teknomovies lakini pia ku subscribe Youtube channel ya DM Online TV

Pages