YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI -2. - teknomovies
YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI -2.

YAFAHAMU MAKUNDI MAWILI MAHASIMU YA HIP HOP NCHINI MAREKANI -2.

Share This
Ilipoishia........

Baada ya muda record label zikaanza kuenea maeneo ya West side ambapo Dr Dre nae akawa na record label ya Death Row Record akiwa na Suge Knight.

Endelea...........

Akiwa na Death Row Record Dr Dre aliachia moja ya album iliyoweka heshima kubwa kwenye muziki wa Hip Hop kwa wakati wote “The Chronic”. Album hii ilileta mapinduzi makubwa na baadhi ya wasanii wakasainiwa kwenye record label yake akiwemo Snoop Doggy Dogg, Tupac Shakur, Warren G, The lady of Rage, Nate Dogg, Daz Dillinger na Kurupt. Hiki kikawa ni kikosi kazi kutoka upande wa magharibi (West Side). Tuone sasa kikosi kazi kutoka East Side.

Kama nilivyokujuza kwenye sehemu ya kwanza kuwa hip hop imezaliwa New York City ambako huku ni East Side kwa maana hiyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema hip hop imeanzia East Coast Side kwani huku ndiko kulikoanza kufanyika DJ’ing, break dancing, MC’ing na graffiti.


B.I.G Notorious
Kiuhalisia East Coast Side walianza lakini walishindwa kujipanga yaani harakati zao za muziki zilikuwa zikifanywa na mmoja mmoja tofauti na West Coast Side ambao wao walikuwa wakifanya  harakati zao za muziki katika makundi hali iliyowafanya waonekane bora kuliko wenzao ambao ndio waanzilishi
Mwaka 1994 mkali kutoka East Coast Side Nas Escobar akaachia Album yake ya Illmatic aliyoirekodi katika studio za Columbia (Columbia Records) baada kusainiwa kwenye studio hiyo akipewa msaada na MC Search. Kwa kuwa Nas alishaanza kujulikana yeye binafsi huku mashabiki wakiwa na hasira za kwanini hawana makundi makubwa kama West Side kwa kina Dre, Dj Premier akaanza kutoa promo kwa makundi pekee ambayo yalikuwepo hapo ingawa hayakuwa na nguvu kwa wakati huo ambayo ni Wu-Tang Clan na Mobb Deep na yakawa kama mhimili kutoka East Side.

P Diddy
Katikati mwa miaka ya 1990’s Bad Boy Records chini ya C.E.O Sean Comb a.k.a Puff Daddy ikaanzishwa ikiwa na Producers kama Hitmen Stevie J, Derick “D Dot” ambao wao wakamshauri mmiliki wa label hiyo waanze na msanii mkali wa Hip Hop kwa kipindi hiko B.I.G Notorious  ambae tayari alikuwa na hits kadhaa. Baada ya kusainiwa kwa B.I.G label ikaanza kuandaa album na baadae wakaachia Album yake ya kwanza “Read To Die” ambayo iliirudisha New York City kwenye midomo ya watu kwa kuzungumzwa kwani ilikuwa ishaanza kupotezwa na West Side kwa kina Dre. 

Tupac- Shakur
Kutokana na mashairi ambayo yalikuwa yakiishambulia kambi pinzani kama mawaki (hawajui kitu) kina Dre nao wakawa wanarudisha makombora kuonesha ni namna gani wanajua game ya Hip Hop….Hapo ikawa katika kila showa lazima wasanii watoke pande zote yani Eat na West na hapo Free Style battle zikawa zinachukua nafasi kwa kiasi kikubwa.


Itaendelea………………..

Usisahau kuacha comment yako na kutufollow Instagram na Twitter @TeknoMovies



No comments:

Post a Comment

Pages