Barakah Da Prince: Msinipangie cha kupost - teknomovies
Barakah Da Prince: Msinipangie cha kupost

Barakah Da Prince: Msinipangie cha kupost

Share This
BAADA ya kupost katika mtandao wake wa Instagram akisifia ngoma mpya ya Diamond Platnumz Hallelujah,  Barakah Da Prince ameoga matusi mazito kutoka kwa mashabiki mbalimbali hasa kutoka timu Kiba wakidai jamaa anajikosha upande wa pili.

Ikumbukwe kuwa, Barakah alikuwa katika kampuni ya Rockstar 4000 kabla ya kujitoa baada ya kutofautiana na AliKiba na hatua yake ya kusapoti wimbo huo imeonekana kama kutaka kujiingiza upande wa pili.

Baada ya kupokea matusi mazito Barakah aliamua kuwatolea povu watu hao baada ya kupost tena picha na akiandika maneno mazito kuwaendea wote wanaomdiss kuwa hawampangii cha kupost.

“Hii page sio ya Mama yako wala Babu yako mpaka unipangie cha kupost Mbuzi pori wewe, Chukua zawadi ya kati mimi nainjoy huku #HALLELUJAH,” aliandika na kumalizia na emoji za kucheka.


“Tatizo hata kukujua sikujui My Friend SOMETIM E,” aliandika katika post ya pili baada ya matusi kuzidi kumiminika zaidi. 
A post shared by AfricanPrince (@barakahtheprince_) on

No comments:

Post a Comment

Pages