Mjue Kwa Uchache Mwanamama Wa Ngwasuma Scarllet Johansson - teknomovies
Mjue Kwa Uchache Mwanamama Wa Ngwasuma Scarllet Johansson

Mjue Kwa Uchache Mwanamama Wa Ngwasuma Scarllet Johansson

Share This
                                               
Anaitwa Scarllet Johansson, Ni Raia Wa Marekani.. Na kazi zake anazofahamika mpaka sasa na watuUlimwengu mzima ni kama Mwigizaji, Mwanamitindo na pia Mwanamuziki.

May Mwaka huu, alitajwa kama mwigizaji wa kike wa muda wote aliyetengeneza mkwanja mrefu zaidi kupitia filamu zake, akiwa kaweza kuingiza dola Bilioni $3.6.

Na mwaka 2016 alitajwa kua ndo mwigizaji wa kike, aliyeingiza mkwanja mrefu zaidi ,akiwa kaingiza dola bilioni $1.6.

Kiusanii mpaka sasa ana album mbili, ambazo ni anyway I Lay My Head ambayo ilitoka mwaka 2008 na nyingine ilikwenda kwa jina la Break Up, ambayo ilitoka mwaka 2009.

Katika uwanja wa filamu rasmi alianza kuonekana katika Luninga kuanzia mwaka 1994 lakini kufahamika sana na watu, ilikua ni kuanzia miaka ya 2000's.

Baadhi ya Filamu AlizoCheza mwanadada huyu ni kama Under the skin, Lucy,The Jungle Book, A love song for Bobby Long, Don Jo, Ghost in the shell na filamu nyingine ambazo umewahi Tazama tofauti na hapo nilizotaja ambazo ulimuona bila kusahau filamu kama Iron man na pia katika mfululizo wa filamu za Avengers akicheza kama Black Widow.
moja ya picha toka filamu yake ya Lucy
                                             Mpaka sasa ana mtoto mmoja aliyepata pamoja na mmiliki wa Independent Agency mfaransa Roman Dauriac.
Lakini katika maisha yake kashatoka na watu kibao sana, mmoja wapo akiwa ni star toka movie Ya Deadpool Ryan Reynolds, ambaye walifikia hatua kwa pamoja ya Kufunga ndoa mwaka 2008,lakini kufikia mpaka mwaka 2011 walitarakiana.
moja ya picha toka filamu ya avengers
                                           Katika mwaka huo huo 2011,Kulitokea na tukio la kusambaa kwa picha za utupu za Kwake, ambapo simu yake ilidukuliwa na baada ya Uchunguzi na FBI walimbaini muhusika wa tukio hilo ambae alisekwa Jela Kwa miaka 10,lakini baada ya miaka mitatu ya tukio hilo, Johansson alikiri Ryan nae kuhusika na tukio hilo Kua picha zilitumwa na yeye pia.

Huyu Ndo Mwanadada, Scarlett, Moja Ya Warembo bora Toka Hollywood, Unaweza ukaacha maoni yako pia Filamu zipi za mwanadada huyu unazozielewa sana tofauti na tajwa hapo juu.

Pages