Muda Huu Tunayo Ninja Assassins Hii Hapa - teknomovies
Muda Huu Tunayo Ninja Assassins Hii Hapa

Muda Huu Tunayo Ninja Assassins Hii Hapa

Share This
Kuna siku niliwaletea stori kuhusu ninja (Maninja)... Na nilisema kila mtu ataje movie yake bora aliyowahi kutazama inayohusu theme ya ninjas.

Na hii ndiyo iliyotajwa Sana na baadhi ya watu waliotoa maoni nami, nimeamua kuisababisha kwa ambao hamjatazama.

Story kwa ufupi... Mzee mr Ozunu, akiongoza ukoo wake wa Ozunu... Aliwachukua watoto yatima kutoka sehemu Mbalimbali duniani, lengo ni kuja kutengeneza kundi La kininja La Mauaji.
Katika kundi hilo alikuepo kijana Raizo ambae yeye tangu akiwa mdogo alikua akila ambush Tu, yote ni kutokana Na mzee ndiye alikua akimuandaa kuja Kurithi kiti chake.

Sasa mzee alikua na mtoto wake wa kike nae alikuepo kwenye kundi hilo la wanafunzi wa mzee na walikua na ka uhusiano na Raizo ka Kimahaba... Lakini mtoto alichoka na maisha hayo ambapo kuna siku aliamua kutoroka na bahati mbaya alikamatwa... Na adhabu yake ilikua kifo.
Kitendo hicho kilimuuzi sana, Raizo ambaye aliapa kuja kulipiza kisasi..kwenye mission yake ya kwanza tu.. Baada ya kukamilisha alikiamsha.. Hivyo kua kwenye hati hati hatari maana aliwindwa hatari.

Utamu wa hii movie, ndani ni kuna kichapo cha nguvu na uzuri zaidi hii imekaa kisasa zaidi tofauti na movies zingine zenye mahadhi ya kininja.

Ilitoka mwezi November tarehe 29 mwaka 2009,na ilitumia Budget $40M
Na mauzo iliweza kuuza $61.6M.

                                     DOWNLOAD NOW

Pages