Huyu Hapa Lil Kim,Rapa Wa Kike Aliyeamua Kujichubua Kama MJ - teknomovies
Huyu Hapa Lil Kim,Rapa Wa Kike Aliyeamua Kujichubua Kama MJ

Huyu Hapa Lil Kim,Rapa Wa Kike Aliyeamua Kujichubua Kama MJ

Share This

Rapper wa kike kutoka marekani,mwanadada Lil Kim leo ni siku yake Ya kuzaliwa ambapo anasheherekea kutimiza miaka 42 leo hii July 11.

Jina lake halisi alilopewa na wazazi wake ni  Kimberly Denise Jones lakini ulimwengu mzima unamfahamu kama Lil kim. Ukiachana na muziki pia ni produza wa nyimbo,mwigizaji, mwandishi wa nyimbo,mwanamitindo na pia ni mwigizaji.

Kama mastaa wengi ambao huanzia chini na kua juu, nae safari yake ilikua hivyo hivyo kwani akiwa na miaka 9 mama na baba walitengana na kupelekea kuishi na baba yake tu ambae hakua na mahusiano nae mazuri jambo lililopelekea akiwa na umri mdogo sana kufukuzwa na baba yake ambapo Lil kim alianza kuishi mtaani na aliacha shule.

Akiwa bado binti mdogo ndipo alikutana na msanii nguli wa Hip Hop Christopher Wallace "Notorious BIG" Ambaye ndiye mtu mpaka sasa Kim anasema hatokuja kumsahau sababu ndiye alikua msaada kwake na pia ndiye aliyemtambulisha katika muziki.

kipindi hicho wakati wanakutana, bado nae BIG hakua maarufu sana,bali alikua ni msanii aliyeanza kuja juu katika miondoko ya muziki wa RAP.

Baada ya BIG kutusua katika game ndipo mwaka 1994 alikuja na kundi la Rap kutoka mitaa huko huko ya Brookylin likifahamika kwa jina la Junior M.A.F.I.A ambapo ndani yake alikuapo Lil kim, ambapo kwa kipindi hicho alikua na umri wa miaka 19.

kundi hilo liliachia albamu moja tu ikienda kwa jina la Conspiracy ambayo ilipata mafanikio mazuri na kuweza kumtambulisha izuri katika ramani ya muziki hiyo ilikua ni mwaka 1995 ambapo albamu ilikua imeachiwa August 29.

mafanikio ya albamu hiyo yalikua mazuri ambapo ilishika nafasi ya 8 katika U.s Billboard 200 na kwa week ya kwanza tu iliweza kuuza kopi 69,000. Desemba 6 mwaka 1995 nyimbo mbili toka albamu hiyo "players anthem pamoja na Get Money" zilikua Certified Gold na baadae Platinum pia.

kufanyika kwa albamu hiyo kulimpa umaarufu pia kwa sana Lil kim ambae nae aliamua kuanza kufanya mziki kama Solo, ambapo mwaka 1996 mwezi Noemba aliachia albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la Hard core ambapo ilikamata nafasi ya 11 katika US Billboard 200 ambapo kwa kipindi hicho aliweka rekodi ya kua mwanamuziki wa kwanza Wa Rap kuweza kufikia nafasi ya juu hiyo.

pia katika Top & RB Albums albamu yake ilikamata nafasi ya 3 na iliweza kuuza kopi 78,000 katika wiki yake ya kwanza na dunia nzima iliuza kopi milioni 5.

Albamu yake ya pili ilienda kwa jina la The Notorious K.I.M ambayo aliichia mwaka 2000 mwezi June tarehe 27 ambapo ilikamata nafasi ya 4 katika Billboard na namba 1 katika Hot billboard na pia kwa wiki ya kwanza tu iliuza kopi 229,000 ambapo baadae ilikuja kua Certified Platinum na RIAA hiyo ikiwa wiki nne mbele baada ya kuachiwa.

mwaka 2003 aliachia albamu yake ya tatu La bella Mafia ambapo ilishika nafasi ya 5 katika chati za Billboard 200 na kwa week ya kwanza tu iliweza kuuza kopi 166,000. mwaka 2005 Kim alipatikana na makosa ya kudanganya kutokana na tukio lilokua limetokea la mashumbulizi ya risasi pamoja na kushiriki katika kufanya uhalifu ambapo alipewa kifungo cha mwaka mmoja  na august 2 mwaka 2006 aliachiwa baada ya kutumikia miezi yake 12.

Baada ya kutoka tu, mwezi septemba aliachia albamu yake ya nne akiipa jina la The naked truth ambayo ilishika nafsi ya 6 katikachati za Billboard na kuuza kopi 109,000 kwa wiki ya kwanza. tena mwaka 2008 mwezi june 3 aliachia mixtape yake iliyokwenda kwa jina la Greatest Of All Time na mwaka 2011 alidondosha mixtape nyingine iliyokwenda kwa jina la Black friday .

Na kwa mwaka 2017 Inategemewa Kim kuja na albamu nyingine ambapo bado hajasema bado jina itaitwaje lakini kwa mwaka huu tayari watu wote waliofanikiwa kupata albamu ya Faith eans pamoja na BIG kuna wimbo unakwenda kwa jina la Lovin you for life ambao kashirikishwa huyu mwanadada.

Kwa upande mwingine Lil kim anafahamika kwa kua na mgogoro na baadhi ya wasanii wenzake kama Foxy Brown ambae mwanzo walikua marafiki lakini mpaka sasa hali ni tete. pia mgogoro wake na rapa mwingine wa kike Eve pia imewahi kutaarifiwa kua Kim alikua na mgogoro na Faith Evans lakini kwa miaka karibuni mgogoro wake na Nicki minaj ndio ambao ulikua umeshika kasi haswaa.

katika upande wa filamu mpaka sasa kashiriki katika filamu zaidi ya 14 ikiwemo filamu inayokwenda kwa jina la Zoolander akiwa na mtaalamu Owen Stilles na filamu nyingine nyingi kama Longshot,she's all that,juwanna mann na nyingine nyingi tu.

ukiachana na hayo mambo mengine, pia Lil kim anafahamika kwa kuwahi kua mmoja wapo ya wasichana waliowahi kudate na BIG lakini mahusiano yao yalikua yakusua sua sana, na mwaka 1999 Lil kim katika interview moja  anasimulia kua alipata ujauzito na BIG ila aliamua kutokuzaa sababu ya namna uhusiano wao kwa kipindi hicho ulivyokua na pia yeye kwa kipindi hicho anasema hakuhitaji mtoto.

Teknomovies Media tunamtakia heri kwake ya kuzaliwa kwa siku ya leo na watu wengine wote mliozaliwa kwa siku ya leo.

Pages