Fast 8, Nyuma Ya Kamera#Fahamu - teknomovies
Fast 8, Nyuma Ya Kamera#Fahamu

Fast 8, Nyuma Ya Kamera#Fahamu

Share This
Leo nimeamua niwasogezee muunganiko wa vipande Mbalimbali toka Filamu iliyofanya vizuri sokoni kwa mwaka huu ya Fast and Furious 8,Ukipenda unaweza ukaiita Fast 8 au The Fate of The Furious. 
                           
Filamu hii, ni ya Nane kutoka toka mfululizo wa Filamu za Fast and furious ambapo Filamu ya kwanza ilitoka Tarehe 22 mwezi June mwaka 2001 ambayo ilitumia Budget Ya kiasi cha dola milioni $38 na sokoni ilifanya vizuri kwa kuweza kuingiza dola milioni $207

Filamu ya pili ilitoka tarehe 6,mwezi June mwaka 2003 ambayo hii ilitumia Budget ya Dola milioni $76 na mauzo kwa dunia nzima yalifikia $236

Filamu ya Tatu, Ilitoka mwaka 2006 nayo ikiwa ni mwezi June tarehe 6..ambayo hii haikufanya vizuri sana  sokoni ambapo iliweza kuuza dola $158M toka bajeti ya dola milioni $85

Filamu ya nne iliachiwa mwezi April mwaka 2009 nayo ilitumia budget $85M na mauzo yaligonga mpaka dola $363M yakipanda juu zaidi.

Filamu ya tano, Ikipewa jina la Fast Five, Hii iliachiwa April 29 mwaka 2011 na mauzo hii iligonga faida nyingi kwa kuweza kuingiza dola milioni $629.9 huku budget ikitumia $160M

Filamu ya sita iliachiwa may 24 mwaka 2013 na mauzo iliweza  kuingiza $788.6M toka budget $160M ikiwa faida kubwa sana imetengenezwa.

Filamu ya saba Iliachiwa April 3 mwaka 2015 ikitumia Budget ya dola milioni $190 na mauzo yaligonga mpaka $1.5 Bilioni.

Ya nane, Ndo hii ambayo utaenda kuangalia matukio nyuma ya Camera, ya kila kitu kilichofanyika... Hii nayo kimafanikio imefanya vizuri sana, kwa kuweza kuuza mpaka sasa $1.2 Bilioni huku Budget ikitumia $250M.

Bonyeza HAPA sasa Kupakua Filamu nzima
Kwa Tathmini hiyo fupi, utakua umeona kwa jinsi, Filamu hii ilivyoweza kuingiza mkwanja mrefu zaidi ambapo ukipiga hesabu Jumla mpaka sasa imeingiza Dola bilioni 5.
Na Bajeti kwa Ujumla ikiwa ni dola Bilioni 1.

                           TAZAMA HAPA CHINI MATUKIO YA NYUMA YA KAMERA,BONYEZA PLAY.


                   

Pages